CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 36
(d) Mwandishi ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka eleza mbinu zozote tatu zilizotumika katika dondoo hili.
From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 3 marks · Topic: Fasihi, Novela
NOVELA (alama 10)
Soma dondoo hii kisha ujibu maswali.
Shule zilipofunguliwa kuanza muhula mpya, Tumaini alijikuta akifanya bidii kama mchwa masomoni. Alitaka kutimiza ndoto yake ya kumaliza masomo ya msingi. Darasa lake sasa lilikuwa tulivu baada ya Majuto kutimuliwa shuleni. Alikuwa kiini cha uovu wote mle darasani. Sasa marafiki zake kama vile Kijungwe walikuja kwa matao ya chini. Bila shaka walipata funzo kutokana na yale yaliyomfika mwenzao. Kwa upande wake, Tumaini hakutia maanani kejeli za wenziwe kutokana na yale yaliyomkumba likizoni. Aliamua kutia komango masikioni ili gubu zao zisiathiri bidii yake masomoni.
Siku moja wakiwa shuleni, Kijungwe alimtania, “Tumaini, hivi uliikimbia tohara kwa sababu ya woga au mchumba uliyechaguliwa hukumpenda?”
Swali hilo lilimkasirisha Tumaini aliyemjibu kwa ukali, “Pilipili iliyo shambani yakuwashiani kikwekwe wewe?”
“Ala! Ukali huo wote ni wa nini? Naskia ulichana mbuga hadi kwa mamako mdogo. Nilidhani wewe ni msichana jasiri sana wala hungeogopa kisu. Au ni wembe?” Kijungwe aliendelea kukejeli.
Huku akiwa ameghadhabika, Tumaini alimrushia Kijungwe jiwe ambalo aliliepa. Jiwe lilifululiza moja kwa moja likampata mwalimu kichwani. Mwalimu huyo aliyekuwa amesimama nje ya darasa, aligeuka huku akijishika kichwa kwa uchungu. Kijungwe alipoona vile alianza kukimbia mara moja lakini mwalimu huyo akamwamuru kusimama. Alimtazama Tumaini aliyekuwa kasimama palepale kama kisiki akishuhudia athari ya jiwe alilorusha.
“Jiwe lile kalirusha nani?” Mwalimu alimwuliza Tumaini.
“Kijungwe,” Tumaini alimjibu bila kicho.
Mwalimu hakutaka kuzisikia kelele za Kijungwe za kujitetea. Aliyaelewa machachari yake, pamoja na mizaha mingi aliyowafanyia wenzake. Kwa hivyo, alimwingiza ofisini na baada ya kumpa onyo kali, alimpa upanga na jembe huku akimwamrisha kwenda kung’oa visiki katika shamba la shule. Siku hiyo Kijungwe hakusoma bali alishinda aking’oa visiki hadi jioni. Tangu wakati huo, Kijungwe alikoma kumkejeli Tumaini.
(d) Mwandishi ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka eleza mbinu zozote tatu zilizotumika katika dondoo hili.
Answer
Tashbihi – "alifanya bidii kama mchwa"; nahau – "kuchana mbuga"; methali / swali la balagha – "Pilipili iliyo shambani yakuwashiani?".
Mbinu na mifano.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- SEHEMU 1: KUSOMA UFAHAMU 1. Ni wito gani uliotolewa na kiongozi kwa ndege wengine? (alama 1)Question 1
- Ndege hawa waliishi kwa kujaliana maslahi. Andika mfano mmoja kutoka kwenye kifungu kubainisha kauli hii. (alama 2)Question 2
- Kwa nini ndege hawakutaabika mafuriko yalipoharibu takriban kila kitu? (alama 1)Question 3
- Eleza funzo linalopatikana katika kifungu hiki. (alama 1)Question 4
- Kwa nini mwandishi anasema kuwa kila mmoja hawezi kuwa mwajiriwa? (alama 1)Question 5
- Mwandishi anasema kuwa vijana na watu wa makamo wanakula mumbi. Hii ni sawa na kusema (alama 1) (wanakula mwata,…Question 6