naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 3

Kwa nini ndege hawakutaabika mafuriko yalipoharibu takriban kila kitu? (alama 1)

From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi 4.
Himaya ya Ndege ilijulikana karibu na mbali kutokana na uwajibikaji wa wote walioishi humo. Kiongozi wao, mbuni, hakusita kuwasifia umuhimu wa kuchanika kwenye mpini ili kuepuka shida zitokanazo na ukosefu. Ndege wengi waliitikia mwito wa kiongozi wao. Kila siku walirauka kabla ya jua kupasua matlai wakaanza shughuli zao za siku. Ungewasikia asubuhi na mapema wakiimba nyimbo za kumtukuza Maulana huku wakikusanya wadudu, matunda, nafaka na utomvu wa maua. Maghala yao yalishiba na kutapika kwani walielewa kuwa akiba haiozi.
Wasemao husema kuwa hakuna mchele ukosao ndume. Tausi alikuwa mmojawapo wa ndege wale lakini mienendo yake ilichukua mkondo tofauti kabisa. Ndege wengine walipojizatiti katika shughuli za kuchuma, kila siku yeye aliteua mavazi maridadi yaliyotiwa nakshi za kila aina. Hapo alipita mbele ya wenzake akijifaragua kwa umaridadi wake. Heroe na Kasuku waliwahi kumwonya mara kadhaa dhidi ya kulaza damu lakini rai zao ziliangukia masikio yaliyotiwa nta.
Wakati mmoja, yalizuka mafuriko makubwa yaliyoharibu takribani kila kitu. Ndege hawakutoka nje kwa kuhofia kupoteza roho zao. Kila mmoja alikaa ndani kwa ndani akila akiba yake. Maskini Tausi! Hakuwa na nafasi ya kujifaragua wala cha kutia mdomoni. Huzuni ilimgubika gubigubi. Ndege wengine walipoona kuwa huenda mwenzao akaangamia, waliamua kumpa msaada wa chakula. Hata hivyo, dhiki alizopitia Tausi zilikuwa funzo tosha kwake.

3. Kwa nini ndege hawakutaabika mafuriko yalipoharibu takriban kila kitu? (alama 1)

Answer

Walikuwa wamejiwekea akiba ya chakula katika maghala yao.

"akiba haiozi".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test