naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 7

Serikali inawajibika kukabiliana na tatizo la uhaba wa kazi. Ni jambo lipi katika kifungu linalothibitisha kauli hii? (alama 2)

From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi 8.
Tatizo la uhaba wa kazi limekuwa donda ndugu katika mataifa mengi. Vijana na watu wa makamo wanakula mumbi kwa kushindwa kutosheleza mahitaji yao kikamilifu. Je, ni nini hasa chanzo cha tatizo hili?
Kwanza, lazima tuelewe kuwa kila mmoja hawezi kuwa mwajiriwa maadamu panahitajika mtu wa kuhudumu na wa kuhudumiwa. Ikiwa sote tutakuwa waajiriwa naye mwajiri atakuwa nani? Ni kwa kutambua jambo hili ambapo serikali imekuwa ikiwahimiza vijana walio shuleni watadarukie kazi za kiufundi ambazo zitawawezesha kuanzisha miradi ya kujitegemea baadaye. Kwa njia hiyo, tutapunguza idadi ya watu wanaong’ang’ania nafasi katika ofisi chache zilizopo.
Hatuna budi kuunga mkono juhudi za serikali. Ikiwa mawazo yetu yataangazia zaidi umuhimu wa kujiajiri kwa kuanzisha vitega uchumi mbalimbali, tutakabiliana na tatizo hilo kikamilifu. Aidha, tuelewe kuwa hakuna kazi yenye hadhi kuliko nyingine; la muhimu ni kipato kipatikanacho katika shughuli yenyewe kwani kazi mbi si mchezo mwema.

7. Serikali inawajibika kukabiliana na tatizo la uhaba wa kazi. Ni jambo lipi katika kifungu linalothibitisha kauli hii? (alama 2)

Answer

Serikali imekuwa ikiwahimiza vijana walio shuleni wajifunze kazi za kiufundi ili waanzishe miradi ya kujitegemea.

Aya ya pili.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test