CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 5
Kwa nini mwandishi anasema kuwa kila mmoja hawezi kuwa mwajiriwa? (alama 1)
From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi 8.
Tatizo la uhaba wa kazi limekuwa donda ndugu katika mataifa mengi. Vijana na watu wa makamo wanakula mumbi kwa kushindwa kutosheleza mahitaji yao kikamilifu. Je, ni nini hasa chanzo cha tatizo hili?
Kwanza, lazima tuelewe kuwa kila mmoja hawezi kuwa mwajiriwa maadamu panahitajika mtu wa kuhudumu na wa kuhudumiwa. Ikiwa sote tutakuwa waajiriwa naye mwajiri atakuwa nani? Ni kwa kutambua jambo hili ambapo serikali imekuwa ikiwahimiza vijana walio shuleni watadarukie kazi za kiufundi ambazo zitawawezesha kuanzisha miradi ya kujitegemea baadaye. Kwa njia hiyo, tutapunguza idadi ya watu wanaong’ang’ania nafasi katika ofisi chache zilizopo.
Hatuna budi kuunga mkono juhudi za serikali. Ikiwa mawazo yetu yataangazia zaidi umuhimu wa kujiajiri kwa kuanzisha vitega uchumi mbalimbali, tutakabiliana na tatizo hilo kikamilifu. Aidha, tuelewe kuwa hakuna kazi yenye hadhi kuliko nyingine; la muhimu ni kipato kipatikanacho katika shughuli yenyewe kwani kazi mbi si mchezo mwema.
5. Kwa nini mwandishi anasema kuwa kila mmoja hawezi kuwa mwajiriwa? (alama 1)
Answer
Kwa sababu wanahitajika waajiri pia; kama sote tutakuwa waajiriwa, hakutakuwa na wa kutuajiri.
Aya ya pili.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Mwandishi anasema kuwa vijana na watu wa makamo wanakula mumbi. Hii ni sawa na kusema (alama 1) (wanakula mwata,…Question 6
- Serikali inawajibika kukabiliana na tatizo la uhaba wa kazi. Ni jambo lipi katika kifungu linalothibitisha kauli hii?…Question 7
- Neno hadhi limetumika katika kifungu. Badala ya neno hilo, mwandishi pia angetumia (alama 1) (hali, umuhimu, heshima,…Question 8
- Andika ujumbe wa aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- “Kuwa na nia pekee hakutoshi kumletea mtu mafanikio. Azma hiyo inapaswa kuandamana na uwajibikaji. Mtu akilaza damu…Question 10
- Fupisha aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11