naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 28

SEHEMU 4: FASIHI (a) Wimbo huu ni wa aina gani?

From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 2 marks · Topic: Fasihi, Nyimbo

Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali.
Kione kitoto aiya aiya
Kitoto kivivu aiya aiya
Hakipendi masomo aiya aiya
Asubuhi chalia aiya aiya.

Kikiwa shuleni aiya aiya
Kila mara kilio aiya aiya
Namtaka mama aiya aiya
Chataka kunyonya aiya aiya.

Mwalimu akifunza aiya aiya
Chazidi kulia aiya aiya
Eti njaa kinahisi aiya aiya
Machozi kapakapa aiya aiya.

Wengine wanasoma aiya aiya
Chataka chakula aiya aiya
Mwalimu mkali aiya aiya
Akipa maonyo aiya aiya.

SEHEMU 4: FASIHI
(a) Wimbo huu ni wa aina gani?

Answer

Wimbo wa watoto (wa kuwaonya / kuwafunza watoto).

Unamhusu kitoto kivivu.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test