naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 31

(d) Hadithi hii inaelezea kuhusu nini? (alama 1)

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Fasihi, Dhamira

FASIHI
28. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, Mulungu aliumba dunia, Binadamu na viumbe wengine walioko. Alipotupa macho alivutiwa sana na uumbaji wake. Alifurahia jinsi Binadamu alivyowajibika kwa kutunza mazingira na kujali maslahi ya viumbe wengine. Alionelea ni vyema ampe tuzo binadamu kutokana na uwajibikaji huo.
Katika makazi ya Mulungu, walikuwemo viumbe wawili aliotumia kama wajumbe. Wa kwanza alikuwa kinyonga. Yeye alitenda mambo taratibu. Mara nyingi, Mulungu alimtumia kufikisha ujumbe uliohitaji mwasilishaji awe makini zaidi. Hata hivyo, kinyonga alikuwa mwenye kigugumizi, ilimhitaji yule aliyemsikiliza awe na subira ya kutosha.
Mjumbe wa pili alikuwa ndege aliyeitwa Kunguru. Huyu alitumwa kupeleka habari za dharura ambazo hazikupaswa kucheleweshwa. Tatizo lake ni kuwa alipenda sana kula. Aidha, alikosa makini akafanya mambo kwa papara.
Kinyonga ndiye aliyetumwa kumpelekea Binadamu taarifa. Mulungu alitaka kumtunuku tunu ya kuishi milele ili aendelee kuutunza ulimwengu. Basi Mulungu akamwambia Kinyonga, “Nenda ukamwambie Binadamu kwamba nimempa uhai wa milele. Kifo kikimwona kitamwondokea mbali”
Kinyonga alifunga safari hadi kwa Binadamu akampashe habari hizo njema. Wakati uo huo, Mnana naye alipewa ujumbe wake apeleke mahali fulani. Wakati wa kurudi, Mnana aliamua kupita kwa Binadamu aone kama kinyonga ameshafikisha taarifa. Alipofika alikuta ndipo mwenzake anang’ang’ana kuwasilisha taarifa.
“Ni....ni...ni-me-tu-tumwa ni...,” akajaribu kusema kinyonga.
Wakati uo huo, Mnana alimkata kalima akasema, “Mulungu amesema kuwa kifo kitakuwa karibu nawe siku zote; hatima yako duniani ni kifo. Jamaa zake wataachiwa majonzi tele.”
Kinyonga alishtuka na kujaribu kumkosoa Mnana. Hata hivyo, Binadamu ambaye hakuwa na subira tena alishajiendea zake baada ya kupokea taarifa ya Mnana.

(d) Hadithi hii inaelezea kuhusu nini? (alama 1)

Answer

Asili ya kifo

Taarifa ya Mnana.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test