CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 35
(b) Eleza masuala mawili ambayo mwandishi ameangazia katika dondoo hili. (alama 2)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 2 marks · Topic: Fasihi, Masuala
29. Tamthilia
Soma dondoo hili kisha ujibu maswali yatakayofuata.
(Mama Halima amekutana na Bi Rahma njiani)
Mama Halima: Hujambo shoga yangu? Unatoka wapi ukitembea haraka hivi.
Bi Rahma: (Akiuwekelea mzigo wake kwenye kisiki kando ya barabara) Sijambo Mama Halima. Nimetoka sokoni kununua vyakula. Wajua siku hizi mvua imeadimika, mashamba yetu hayatoi chochote. Hata nawangoja wageni wangu kesho nione kama mambo yatabadilika kidogo.
Mama Halima: (Akitazama huku na kule kuhakikisha kuwa wapiti njia wengine hawatamsikia) Kweli shoga yangu umeamua kumwachisha Rehema shule akaolewe? Rehema ni msichana mwerevu. Naona umekosa mwelekeo rafiki yangu.
Bi Rahma: (Akishusha uso wa aibu) Tatizo ni mume wangu ambaye ameshikilia mila potovu za kijadi. Sijui kama ni umaskini umemfumba macho.
Mama Halima: Wewe kama mzazi mwenzake unakubaliana naye?
Bi Rahma: Nikubaliane vipi na mipango hiyo dufu? Sitaki Rehema apitie yale niliyopitia. Nataka asome hadi chuo kikuu angaa apate kazi. Kwa njia hiyo, atakata minyororo ya umaskini katika familia yetu.
Mama Halima: (Akimshika mkono) kama ni hivyo, chukua mzigo wako unifuate.
(Wanafika katika ofisi ya Chifu)
Wote pamoja: Hujambo Bwana Chifu?
Chifu: Sijambo? Karibuni, ni lipi limewaleta wakati huu tunapokaribia kufunga ofisi.
Mama Halima: Nimekuja kushtaki dhuluma zinazofanyika katika kijiji ninachowakilisha. Huyu hapa ni Bi Rahma. Mumewe ameamua kumwachisha masomo bintiye ili amwoze.
Chifu: (Anatoa shajara yake na kuanza kuandika) Lo! Mbona watu wengine wangali wanaselea katika mila zilizopitwa na wakati? Hata kama mwacha mila ni mtumwa, binadamu hafai kuwa kipofu mithili ya jongoo. Je, mipango hiyo itafanyika lini?
Bi Rahma: Wageni wanatarajiwa hapo kesho alasiri.
Chifu: (Akimgeukia Mama Halima) Kesho nitafika hapo kijijini. Lazima tulivalie njugu suala hili. Hata hivyo msiseme lolote kwanza.
Mama Halima: Usiwe na wasiwasi kiongozi wetu. Tutafyata ndimi zetu ipasavyo. Kesho tutakusubiri kwa hamu na ghamu.
Chifu: Haya, mnaweza kuondoka.
Wote wawili: Kwaheri Bwana Chifu.
Chifu: Kwaheri ya kuonana.
(b) Eleza masuala mawili ambayo mwandishi ameangazia katika dondoo hili. (alama 2)
Answer
Ndoa za mapema – Rehema anaozwa; umaskini – unamsukuma baba yake amwoze.
Mambo yanayojadiliwa.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (c) Fafanua sifa mbili za Mama Halima kulingana na dondoo hili. (alama 2)Question 36
- (d) Haki za watoto zimezingatiwa vipi katika dondoo hili? (alama 1)Question 37
- (e) Huku ukitolea mifano mwafaka, jadili mbinu zozote tatu za lugha ambazo mwandishi wa dondoo hili ametumia. (alama 3)Question 38
- Kifaru alikuwa kiongozi wa wapi? (alama 1)Question 1
- Kwa nini wanyama walihudhuria mkutano? (alama 1)Question 2
- Kama Chui asingetoroka, nini kingemtokea? (alama 1)Question 3