naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 34

(a) Taja aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 2 marks · Topic: Fasihi, Mandhari

29. Tamthilia
Soma dondoo hili kisha ujibu maswali yatakayofuata.
(Mama Halima amekutana na Bi Rahma njiani)
Mama Halima: Hujambo shoga yangu? Unatoka wapi ukitembea haraka hivi.
Bi Rahma: (Akiuwekelea mzigo wake kwenye kisiki kando ya barabara) Sijambo Mama Halima. Nimetoka sokoni kununua vyakula. Wajua siku hizi mvua imeadimika, mashamba yetu hayatoi chochote. Hata nawangoja wageni wangu kesho nione kama mambo yatabadilika kidogo.
Mama Halima: (Akitazama huku na kule kuhakikisha kuwa wapiti njia wengine hawatamsikia) Kweli shoga yangu umeamua kumwachisha Rehema shule akaolewe? Rehema ni msichana mwerevu. Naona umekosa mwelekeo rafiki yangu.
Bi Rahma: (Akishusha uso wa aibu) Tatizo ni mume wangu ambaye ameshikilia mila potovu za kijadi. Sijui kama ni umaskini umemfumba macho.
Mama Halima: Wewe kama mzazi mwenzake unakubaliana naye?
Bi Rahma: Nikubaliane vipi na mipango hiyo dufu? Sitaki Rehema apitie yale niliyopitia. Nataka asome hadi chuo kikuu angaa apate kazi. Kwa njia hiyo, atakata minyororo ya umaskini katika familia yetu.
Mama Halima: (Akimshika mkono) kama ni hivyo, chukua mzigo wako unifuate.
(Wanafika katika ofisi ya Chifu)
Wote pamoja: Hujambo Bwana Chifu?
Chifu: Sijambo? Karibuni, ni lipi limewaleta wakati huu tunapokaribia kufunga ofisi.
Mama Halima: Nimekuja kushtaki dhuluma zinazofanyika katika kijiji ninachowakilisha. Huyu hapa ni Bi Rahma. Mumewe ameamua kumwachisha masomo bintiye ili amwoze.
Chifu: (Anatoa shajara yake na kuanza kuandika) Lo! Mbona watu wengine wangali wanaselea katika mila zilizopitwa na wakati? Hata kama mwacha mila ni mtumwa, binadamu hafai kuwa kipofu mithili ya jongoo. Je, mipango hiyo itafanyika lini?
Bi Rahma: Wageni wanatarajiwa hapo kesho alasiri.
Chifu: (Akimgeukia Mama Halima) Kesho nitafika hapo kijijini. Lazima tulivalie njugu suala hili. Hata hivyo msiseme lolote kwanza.
Mama Halima: Usiwe na wasiwasi kiongozi wetu. Tutafyata ndimi zetu ipasavyo. Kesho tutakusubiri kwa hamu na ghamu.
Chifu: Haya, mnaweza kuondoka.
Wote wawili: Kwaheri Bwana Chifu.
Chifu: Kwaheri ya kuonana.

(a) Taja aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)

Answer

Barabarani na ofisini mwa Chifu.

Wanapokutana na wanapokwenda.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test