naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 20

Umuhimu wa hospitali ni upi kulingana na mazungumzo hayo?

From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 19 mpaka la 25.

(Shawe anazungumza na baba yake sebuleni)

Shawe: Baba, shuleni tunaambiwa kuwa zamani watu walikuwa na afya nzuri kuliko sasa. Je, hayo yaliwezekanaje ilhali huduma za matibabu hazikuwa zimeimarika kama zilivyo sasa?

Baba: (Akisafisha koo) Hilo ni swali zuri. Kwanza lazima uelewe kuwa hospitali hutumika aghalabu kurudisha afya iliyodhoofika. Yafaa tuzuie madhara mapema kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Shawe: Enhee! Ni mambo yapi yanayofanywa ambayo hayasaidii kutunza afya?

Baba: Hapo jadi, watu walifurahia sana kula vyakula vya kiasili kama wimbi, muhogo, viazivikuu na mboga za kiasili. Badala ya kula nyama kwa wingi, walitumia maharagwe, pojo na mbaazi. Je, ulaji wa siku hizi unazingatia hayo?

Shawe: La! Watu wanapendelea vyakula vyenye mafuta mengi kama chipsi kwa kuku na vyenye sukari mathalani keki, pipi na biskuti. Si ajabu kuwa siha zetu zinadorora.

Baba: Kweli kabisa! Zaidi ya yote watu wa hapo awali walitunza mienendo yao; kinyume na hali ilivyo. Hawakushiriki ulevi wa kupindukia, mapenzi ya kiholela wala vita tunavyoshuhudia kila mahali.

Shawe: Shabash! Nimejifunza mengi leo. Nimegundua kuwa afya bora inamhitaji mtu kujistahi na kuandama mienendo inayofaa. Asante baba.

20. Umuhimu wa hospitali ni upi kulingana na mazungumzo hayo?

  1. AKuzuia shida za kiafya.
  2. BKufunza watu kujiepusha na maradhi.
  3. CKueleza madhara ya magonjwa katika jamii.
  4. DKuondoa madhara ya kiafya mwilini.

Answer

D. Kuondoa madhara ya kiafya mwilini.

Baba anasema hospitali hutumika aghalabu kurudisha afya iliyodhoofika, yaani kutibu madhara yaliyokwisha kumpata mtu. Kuzuia ni jukumu letu kabla ya kufika hospitalini.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test