CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 23
Neno 'shabash' ni aina ya
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Sarufi na Matumizi ya Lugha, Aina za Maneno
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 19 mpaka la 25.
(Shawe anazungumza na baba yake sebuleni)
Shawe: Baba, shuleni tunaambiwa kuwa zamani watu walikuwa na afya nzuri kuliko sasa. Je, hayo yaliwezekanaje ilhali huduma za matibabu hazikuwa zimeimarika kama zilivyo sasa?
Baba: (Akisafisha koo) Hilo ni swali zuri. Kwanza lazima uelewe kuwa hospitali hutumika aghalabu kurudisha afya iliyodhoofika. Yafaa tuzuie madhara mapema kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Shawe: Enhee! Ni mambo yapi yanayofanywa ambayo hayasaidii kutunza afya?
Baba: Hapo jadi, watu walifurahia sana kula vyakula vya kiasili kama wimbi, muhogo, viazivikuu na mboga za kiasili. Badala ya kula nyama kwa wingi, walitumia maharagwe, pojo na mbaazi. Je, ulaji wa siku hizi unazingatia hayo?
Shawe: La! Watu wanapendelea vyakula vyenye mafuta mengi kama chipsi kwa kuku na vyenye sukari mathalani keki, pipi na biskuti. Si ajabu kuwa siha zetu zinadorora.
Baba: Kweli kabisa! Zaidi ya yote watu wa hapo awali walitunza mienendo yao; kinyume na hali ilivyo. Hawakushiriki ulevi wa kupindukia, mapenzi ya kiholela wala vita tunavyoshuhudia kila mahali.
Shawe: Shabash! Nimejifunza mengi leo. Nimegundua kuwa afya bora inamhitaji mtu kujistahi na kuandama mienendo inayofaa. Asante baba.
23. Neno 'shabash' ni aina ya
- Akihusishi
- Bkiwakilishi
- Ckiingizi
- Dkivumishi.
Answer
C. kiingizi
Shabash ni neno linaloonyesha hisia ya kufurahia au kusifu. Maneno ya aina hii ni vihisishi, ambavyo pia huitwa viingizi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ni maradhi yapi hayasababishwi na mapenzi ya kiholela?Question 24
- 'Kujistahi' kulingana na kifungu niQuestion 25
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 27.Question 27
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 28.Question 28
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 29.Question 29