naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 19

Shawe alitaka kujua nini kutoka kwa baba yake?

From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 19 mpaka la 25.

(Shawe anazungumza na baba yake sebuleni)

Shawe: Baba, shuleni tunaambiwa kuwa zamani watu walikuwa na afya nzuri kuliko sasa. Je, hayo yaliwezekanaje ilhali huduma za matibabu hazikuwa zimeimarika kama zilivyo sasa?

Baba: (Akisafisha koo) Hilo ni swali zuri. Kwanza lazima uelewe kuwa hospitali hutumika aghalabu kurudisha afya iliyodhoofika. Yafaa tuzuie madhara mapema kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Shawe: Enhee! Ni mambo yapi yanayofanywa ambayo hayasaidii kutunza afya?

Baba: Hapo jadi, watu walifurahia sana kula vyakula vya kiasili kama wimbi, muhogo, viazivikuu na mboga za kiasili. Badala ya kula nyama kwa wingi, walitumia maharagwe, pojo na mbaazi. Je, ulaji wa siku hizi unazingatia hayo?

Shawe: La! Watu wanapendelea vyakula vyenye mafuta mengi kama chipsi kwa kuku na vyenye sukari mathalani keki, pipi na biskuti. Si ajabu kuwa siha zetu zinadorora.

Baba: Kweli kabisa! Zaidi ya yote watu wa hapo awali walitunza mienendo yao; kinyume na hali ilivyo. Hawakushiriki ulevi wa kupindukia, mapenzi ya kiholela wala vita tunavyoshuhudia kila mahali.

Shawe: Shabash! Nimejifunza mengi leo. Nimegundua kuwa afya bora inamhitaji mtu kujistahi na kuandama mienendo inayofaa. Asante baba.

19. Shawe alitaka kujua nini kutoka kwa baba yake?

  1. AUmuhimu wa kuwa na afya bora.
  2. BJinsi ya kutunza afya.
  3. CMatibabu ya kisasa.
  4. DJinsi alivyoishi zamani.

Answer

B. Jinsi ya kutunza afya.

Shawe aliuliza jinsi watu wa zamani walivyokuwa na afya nzuri, na ni mambo yapi yasiyosaidia kutunza afya: alitaka kujua jinsi ya kutunza afya.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test