CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 15
Tendo la mti kuharibu mali ya Sungura
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 11 mpaka 18.
Sungura na Nyani walikuwa majirani. Mola aliwajalia neema sana katika shughuli zao. Sungura alikuwa mfugaji hodari. Mazizi yake yalijaa na kutapika ng’ombe wa maziwa, mafahali, beberu na mbarika, kondoo na wanyama wengine chungu nzima. Nyani kwa upande wake alikuwa maarufu katika kilimo cha mimea. Alishiriki kilimo biashara na kukuza mimea mingine kwa matumizi ya aila yake. Ufanisi wa wanyama hao uliwafanya majirani zao kuwahusudu sana.
Siku moja, ng'ombe wa Sungura waliingia shambani mwa Nyani kimakosa wakaharibu mimea. Nyani alipoyashuhudia hayo alipandwa na mori mithili ya mbogo aliyejeruhiwa. Huyoo! Alichukua bakora akawacharaza mifugo hao akiwaelekeza kwa mtemi. Alifungua mashtaka dhidi ya jirani yake. Jitihada za Sungura za kujitetea na kuonyesha kuwa tukio hilo halikutokea kwa makusudi ziliangukia masikio yaliyotiwa nta. Mtemi alitoa hukumu yake, Sungura akamlipa Nyani fidia kubwa.
Sungura alirudi manzilini akisononeka moyoni. Alishindwa kwa nini jirani yake hakutaka kumsikiliza. Akiwa na dukuduku hilo alikaa akasubiri nafasi ya kulipiza kisasi. Ama kweli, mhini na mhiniwa njia yao ni moja. Hazikupita siku nyingi, mwembe mkubwa uliokuwa katika shamba la Nyani, karibu na mpaka wake na Sungura ukaangushwa na upepo. Mti huu uliharibu kabisa kizimba cha kuku, ukawaua ndege kadhaa na kuwajeruhi ng’ombe waliokuwa hapo karibu. Badala ya kuhuzunika, Sungura aliangua kicheko kikubwa akielekea kwa mtemi kupeleka taarifa.
Siku iliyofuata, majirani hao walijipata tena katika ukumbi wa mtemi, Sungura akililia haki yake. Jaribio la Nyani la kuonyesha kuwa tukio hilo lilikuwa la kimaumbile, kwani mti haukuanguka kwa kukatwa, halikufaa kitu. Uamuzi ulitolewa Nyani amlipe Sungura. Ilimbidi auze nafaka yote iliyokuwa katika maghala yake na kuchukua mkopo kutoka kwa Tembo ili apate pesa alizodaiwa. Sungura hakupigwa na mshipa licha ya dhiki za mwenzake.
Kabla ya kufumukana, Mzee Kobe aliyekuwa miongoni mwa hadhira aliomba nafasi ya kuzungumza. “Ndugu zangu,” akaanza, “hatufai kuendelea kuishi hivi. Tusipodhibiti hisia kama wivu, hasira, chuki na kisasi tutabomoa mshikamano wa jamii yetu. Je, hali ikiwa hivyo, ni nani atakayemfaa mwenzake?” Baada ya kusema hayo, Mzee Kobe aliuchukua mkongojo wake na kuondoka kwa ule mwendo wake wa kawaida.
Wote waliokuwepo walitazamana bila kusema lolote. Sungura na Nyani walishindwa kutazamana kwa aibu. Walijongeleana taratibu, wakakumbatiana huku machozi ya majonzi yakiwadondoka ndondondo!
15. Tendo la mti kuharibu mali ya Sungura
- Alilikuwa bahati mbaya tu
- Blilipangwa na Nyani
- Clilipangwa na Sungura mwenyewe
- Dlilikuwa la kulipiza kisasi.
Answer
A. lilikuwa bahati mbaya tu
Mwembe uliangushwa na upepo; haukukatwa na mtu yeyote, kwa hiyo ilikuwa bahati mbaya.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini Sungura aliangua kicheko?Question 16
- Kulingana na kifungu, mshikamano wa kijamii huvurugwa zaidi naQuestion 17
- Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya niQuestion 18
- Shawe alitaka kujua nini kutoka kwa baba yake?Question 19
- Umuhimu wa hospitali ni upi kulingana na mazungumzo hayo?Question 20
- Mienendo inayoathiri afya kulingana na kifungu niQuestion 21