CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 9
(b) Eleza hatua mbili ambazo Katana alichukua baada ya kugundua kuwa ni mhanga wa uhalifu wa mtandaoni. (Alama 2)
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 2 marks · Topic: Fasihi, Wahusika
ZOEZI 3: NOVELLA (ALAMA 10)
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali yanayofuata.
Asubuhi moja ya Jumatatu, Katana aliamka mapema kwa shauku ya kuanza wiki mpya shuleni.
Alipofungua simu yake, alikumbana na jumbe nyingi zisizopendeza zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Picha zake zilizotengenezwa kwa udanganyifu zilikuwa zikisambazwa na wanafunzi kadhaa.
Alijawa na huzuni na aibu kubwa. Alihisi dunia ikimlemea.
Katika harakati za kutafuta usaidizi, alielekea kwa mwalimu wa mwongozo na ushauri ambaye alimshauri kuripoti tukio hilo kwa idara ya usalama wa mitandaoni. Katana alifanya hivyo na baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa mwanafunzi mwenzake, Dida, ndiye aliyetekeleza uhalifu huo wa mtandaoni. Dida aliadhibiwa vikali kwa kuvunja sheria za matumizi salama ya mtandao.
Katana alipata faraja na msaada wa kiakili, huku shule ikianzisha kampeni ya kuelimisha wanafunzi kuhusu usalama wa mitandaoni na athari za uhalifu wa aina hiyo.
(b) Eleza hatua mbili ambazo Katana alichukua baada ya kugundua kuwa ni mhanga wa uhalifu wa mtandaoni. (Alama 2)
Answer
Alimtafuta mwalimu wa ushauri nasaha; aliripoti tukio kwa idara ya usalama wa mitandaoni.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (c) Fafanua masuala mawili ya kijamii yanayoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)Question 10
- (d) Eleza ujumbe mmoja muhimu unaopatikana katika sehemu hii ya novela. (Alama 1)Question 11
- (e) Taja vipengele viwili vya lugha vilivyotumika katika sehemu hii ya novela na kueleza matumizi yake. (Alama 2)Question 12
- (f) Kwa nini shule iliamua kuanzisha kampeni ya kuelimisha kuhusu usalama wa mtandaoni? (Alama 1)Question 13
- (a) Tathmini mchango wa ploti katika sehemu hii ya tamthilia katika kukuza dhamira kuu. (Alama 2)Question 14
- (b) Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia? (Alama 1)Question 15