CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 11
(d) Eleza ujumbe mmoja muhimu unaopatikana katika sehemu hii ya novela. (Alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 1 mark · Topic: Fasihi, Ujumbe
ZOEZI 3: NOVELLA (ALAMA 10)
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali yanayofuata.
Asubuhi moja ya Jumatatu, Katana aliamka mapema kwa shauku ya kuanza wiki mpya shuleni.
Alipofungua simu yake, alikumbana na jumbe nyingi zisizopendeza zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Picha zake zilizotengenezwa kwa udanganyifu zilikuwa zikisambazwa na wanafunzi kadhaa.
Alijawa na huzuni na aibu kubwa. Alihisi dunia ikimlemea.
Katika harakati za kutafuta usaidizi, alielekea kwa mwalimu wa mwongozo na ushauri ambaye alimshauri kuripoti tukio hilo kwa idara ya usalama wa mitandaoni. Katana alifanya hivyo na baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa mwanafunzi mwenzake, Dida, ndiye aliyetekeleza uhalifu huo wa mtandaoni. Dida aliadhibiwa vikali kwa kuvunja sheria za matumizi salama ya mtandao.
Katana alipata faraja na msaada wa kiakili, huku shule ikianzisha kampeni ya kuelimisha wanafunzi kuhusu usalama wa mitandaoni na athari za uhalifu wa aina hiyo.
(d) Eleza ujumbe mmoja muhimu unaopatikana katika sehemu hii ya novela. (Alama 1)
Answer
Tunapaswa kutumia mtandao kwa usalama na kuwajibika.
Kilichompata Dida na Katana.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (e) Taja vipengele viwili vya lugha vilivyotumika katika sehemu hii ya novela na kueleza matumizi yake. (Alama 2)Question 12
- (f) Kwa nini shule iliamua kuanzisha kampeni ya kuelimisha kuhusu usalama wa mtandaoni? (Alama 1)Question 13
- (a) Tathmini mchango wa ploti katika sehemu hii ya tamthilia katika kukuza dhamira kuu. (Alama 2)Question 14
- (b) Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia? (Alama 1)Question 15
- (c) Taja sifa mbili zinazoonyesha kuwa kifungu hiki ni mfano wa tamthilia. (Alama 2)Question 16
- (d) Taja maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 17