naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 12

(e) Taja vipengele viwili vya lugha vilivyotumika katika sehemu hii ya novela na kueleza matumizi yake. (Alama 2)

From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 2 marks · Topic: Fasihi, Lugha

ZOEZI 3: NOVELLA (ALAMA 10)
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali yanayofuata.
Asubuhi moja ya Jumatatu, Katana aliamka mapema kwa shauku ya kuanza wiki mpya shuleni.
Alipofungua simu yake, alikumbana na jumbe nyingi zisizopendeza zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Picha zake zilizotengenezwa kwa udanganyifu zilikuwa zikisambazwa na wanafunzi kadhaa.
Alijawa na huzuni na aibu kubwa. Alihisi dunia ikimlemea.
Katika harakati za kutafuta usaidizi, alielekea kwa mwalimu wa mwongozo na ushauri ambaye alimshauri kuripoti tukio hilo kwa idara ya usalama wa mitandaoni. Katana alifanya hivyo na baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa mwanafunzi mwenzake, Dida, ndiye aliyetekeleza uhalifu huo wa mtandaoni. Dida aliadhibiwa vikali kwa kuvunja sheria za matumizi salama ya mtandao.
Katana alipata faraja na msaada wa kiakili, huku shule ikianzisha kampeni ya kuelimisha wanafunzi kuhusu usalama wa mitandaoni na athari za uhalifu wa aina hiyo.

(e) Taja vipengele viwili vya lugha vilivyotumika katika sehemu hii ya novela na kueleza matumizi yake. (Alama 2)

Answer

Lugha ya hisia – kuonyesha huzuni na aibu ya Katana ("Alijawa na huzuni"); tashihisi – "Alihisi dunia ikimlemea" kuonyesha uzito wa tatizo.

Vipengele pamoja na matumizi.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test