CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 14
(a) Tathmini mchango wa ploti katika sehemu hii ya tamthilia katika kukuza dhamira kuu. (Alama 2)
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 2 marks · Topic: Fasihi, Ploti
ZOEZI 4: TAMTHILIA (ALAMA 10)
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali:
Sehemu ya 1
(Onyesho la 1)
(Nia na Amani wanakaa kwenye kivuli cha mti mkubwa. Hali ya hewa ni ya joto na wanajadili kuhusu maisha yao.)
Nia: Amani, kuna wakati najiuliza kama tunafanya vya kutosha kwa jamii yetu. Inavyoonekana, watu wanashughulika na mambo yao tu, na hakuna mtu anayewajibika kusaidia wengine.
Amani: Ni kweli Nia, lakini ni vipi tutakavyobadilisha hali hii? Watu wengi wanahitaji msaada, lakini kila mmoja anaangalia maslahi yake mwenyewe.
Nia: Nadhani tunahitaji kuhamasisha watu kuwa na huruma na wengine, lakini pia lazima tuanze kwa kubadilika sisi wenyewe.
Amani: Hilo ni jambo muhimu. Hatuwezi kutarajia mabadiliko kutoka kwa wengine kama sisi wenyewe hatuonyeshi mfano mzuri.
Nia: (Akizungumza kwa sauti kubwa) Huu ni wakati wa kuungana na kusaidiana kama jamii!
(a) Tathmini mchango wa ploti katika sehemu hii ya tamthilia katika kukuza dhamira kuu. (Alama 2)
Answer
Inaonyesha tatizo la jamii (watu kutojali wengine) kisha inaonyesha suluhisho la kuhamasisha mshikamano.
Mwanzo na mwisho wa mazungumzo.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (b) Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia? (Alama 1)Question 15
- (c) Taja sifa mbili zinazoonyesha kuwa kifungu hiki ni mfano wa tamthilia. (Alama 2)Question 16
- (d) Taja maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 17
- (e) Taja kipengele kimoja cha lugha kilichotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 1)Question 18
- (f) Eleza ujumbe mmoja unaoibuka kutokana na mazungumzo kati ya Nia na Amani. (Alama 2)Question 19
- SEHEMU YA A: KUANDIKA (alama 15) Andika insha inayozungumzia “mambo muhimu ya kuzingatia ili kuepuka uhalifu wa…Question 1