naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 24

Chagua neno ambalo Pendo angetumia katika nafasi ya 24 kwenye mazungumzo.

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 21 hadi la 25.
(Ni katika maabara ya shule. Wanafunzi wamevaa mavazi ya kinga. Pendo na Sifa wanafanya majaribio ya sayansi huku wakiongea kwa sauti ya chini.)
Pendo: (Akigeuka kumtazama mwenzake.) Mambo vipi Sifa?
Sifa: Shwari kabisa rafiki yangu. Nawe unaendeleaje na mchanganyiko wako?
Pendo: (Kwa tabasamu.) __21__ Nashughulikia jaribio la kemia. Si unajua ni matayarisho ya maonyesho ya kitaifa ya sayansi? Kundi letu linajitahidi kwa udi na uvumba. Unajua, dau la mnyonge huenda
Sifa: (Akidakia.) Joshoni, kweli. Hata sisi hatulali fofofo. Mwaka uliopita tulishika nafasi ya pili. Safari hii tumedhamiria kuibuka washindi wa kwanza kabisa. Wasichana wote wamesema liwe liwalo, tuzo ni yetu.
Pendo: (Akihema kwa uchovu.) Safi sana! Kwa upande wa wavulana, hawachezi mbali. Wameamua kuwa mwaka huu lazima wajivunie mafanikio yao baada ya kuteleza mara ya mwisho.
Sifa: (Akipunguza kasi ya kuchanganya dawa.) Ngoja nitulie kidogo. Nimesimama kwa saa kadhaa; miguu yangu inaanza kuniuma. Nikizidi hivi nitalegalega.
Pendo: (Akisimama.) __24__ Hakika, mapumziko ni muhimu ili kurejesha nguvu. Kwaheri kwa sasa. Tutaonana wakati wa chakula cha mchana.
Sifa: (Akimpungia mkono.) Nami nitatokea huko punde si punde. (Wanaagana.)

24. Chagua neno ambalo Pendo angetumia katika nafasi ya 24 kwenye mazungumzo.

  1. ABasi
  2. BPole
  3. CSamahani
  4. DHongera

Answer

B. Pole

Sifa analalamika miguu kuuma.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test