CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 23
Ni yepi kati ya maneno yafuatayo yanayoonyesha kuwa wahusika walikuwa na uhusiano wa karibu?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 21 hadi la 25.
(Ni katika maabara ya shule. Wanafunzi wamevaa mavazi ya kinga. Pendo na Sifa wanafanya majaribio ya sayansi huku wakiongea kwa sauti ya chini.)
Pendo: (Akigeuka kumtazama mwenzake.) Mambo vipi Sifa?
Sifa: Shwari kabisa rafiki yangu. Nawe unaendeleaje na mchanganyiko wako?
Pendo: (Kwa tabasamu.) __21__ Nashughulikia jaribio la kemia. Si unajua ni matayarisho ya maonyesho ya kitaifa ya sayansi? Kundi letu linajitahidi kwa udi na uvumba. Unajua, dau la mnyonge huenda
Sifa: (Akidakia.) Joshoni, kweli. Hata sisi hatulali fofofo. Mwaka uliopita tulishika nafasi ya pili. Safari hii tumedhamiria kuibuka washindi wa kwanza kabisa. Wasichana wote wamesema liwe liwalo, tuzo ni yetu.
Pendo: (Akihema kwa uchovu.) Safi sana! Kwa upande wa wavulana, hawachezi mbali. Wameamua kuwa mwaka huu lazima wajivunie mafanikio yao baada ya kuteleza mara ya mwisho.
Sifa: (Akipunguza kasi ya kuchanganya dawa.) Ngoja nitulie kidogo. Nimesimama kwa saa kadhaa; miguu yangu inaanza kuniuma. Nikizidi hivi nitalegalega.
Pendo: (Akisimama.) __24__ Hakika, mapumziko ni muhimu ili kurejesha nguvu. Kwaheri kwa sasa. Tutaonana wakati wa chakula cha mchana.
Sifa: (Akimpungia mkono.) Nami nitatokea huko punde si punde. (Wanaagana.)
23. Ni yepi kati ya maneno yafuatayo yanayoonyesha kuwa wahusika walikuwa na uhusiano wa karibu?
- AMwaka uliopita tulishika nafasi
- BShwari kabisa rafiki yangu
- CKundi letu linajitahidi
- DNami nitatokea huko punde
Answer
B. Shwari kabisa rafiki yangu
"rafiki yangu".
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Chagua neno ambalo Pendo angetumia katika nafasi ya 24 kwenye mazungumzo.Question 24
- Ni ishara gani ambayo Pendo alistahili kutumia alipomuaga Sifa?Question 25
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 27.Question 27
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 28.Question 28
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 29.Question 29