CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
Eleza maana ya usaili kama lilivyotumika katika taarifa
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali la 1 - 7.
Mambo yanayohusu shule na maisha ya kijamii yanaweza wakati mwingine kuchangia msukumo ambao unaweza kuwazidi watoto. Lakini wanaweza kusaidiwa kujenga njia nzuri za kukabiliana na msongo na kusuluhisha shida zao kila siku.
Shirika moja la utafiti kule marekani linasema kuwa watoto husuluhisha msongo kwa njia nzuri au mbaya. Pia laelezea kuwa huku wakiwa hawawezi kuzungumzia kile kinachowasumbua watoto hutaka kuwafikia wazazi wao ili kupata msaada kushinda matatizo yao. Kwa kawaida si rahisi kwa wazazi kujua wafanye nini watoto wao wanaposhikwa na msongo.
Ni vyema kumwambia mtoto kuwa umegundua jambo ambalo linamsumbua. Ikiwezekana, taja hisia ambazo unadhani zinamtatiza mtoto. Hii haifai kuwa kama shutuma. Hii ni njia ya kawaida ya mtazamo kuwa unavutiwa na kutaka kusikia mengi yanayomkera mtoto. Kuwa mwenye huruma na umwonyeshe kuwa unajali na kutafakari hali yake.
Ni vizuri kumsikiliza mtoto. Msikilize kwa makini na utulivu na hamu kuu. Kuwa na uwazi na mapenzi. Epuka kuwa na tamaa ya kuhukumu, kumkemea ama kusema vile unafikiri mtoto anafaa kufanya. Hapo wazo ni kuzipa hisia za mtoto nafasi ya kusikika. Jaribu kupata habari yote kwa njia ya usaili.
7. Eleza maana ya usaili kama lilivyotumika katika taarifa
- Akujidadisi kwa kujiuliza maswali.
- Bkufanya mahojiano kwa kuuliza maswali.
- Ckuandika maswali mtoto ajibu.
- Dkumkemea mtoto ili azungumze.
Answer
B. kufanya mahojiano kwa kuuliza maswali.
Usaili ni mahojiano: kupata habari kwa kuuliza maswali.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Katika aya ya kwanza mwandishi anakubaliana kuwaQuestion 8
- Dhamira hasa ya walioanzisha uundaji na uuzaji wa sehemu mbalimbali za mwili ilikuwaQuestion 9
- Sehemu zifuatazo zinanunuliwa kulingana na ufahamu isipokuwaQuestion 10
- Methali ifuatayo imetumiwa katika ufahamu isipokuwaQuestion 11
- Aghalabu msusi,Question 12
- Wanaobadilisha au kugeuza rangi za miliQuestion 13