naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Kwa nini ni vibaya kutoa hukumu kwa mtoto?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali la 1 - 7.
Mambo yanayohusu shule na maisha ya kijamii yanaweza wakati mwingine kuchangia msukumo ambao unaweza kuwazidi watoto. Lakini wanaweza kusaidiwa kujenga njia nzuri za kukabiliana na msongo na kusuluhisha shida zao kila siku.

Shirika moja la utafiti kule marekani linasema kuwa watoto husuluhisha msongo kwa njia nzuri au mbaya. Pia laelezea kuwa huku wakiwa hawawezi kuzungumzia kile kinachowasumbua watoto hutaka kuwafikia wazazi wao ili kupata msaada kushinda matatizo yao. Kwa kawaida si rahisi kwa wazazi kujua wafanye nini watoto wao wanaposhikwa na msongo.

Ni vyema kumwambia mtoto kuwa umegundua jambo ambalo linamsumbua. Ikiwezekana, taja hisia ambazo unadhani zinamtatiza mtoto. Hii haifai kuwa kama shutuma. Hii ni njia ya kawaida ya mtazamo kuwa unavutiwa na kutaka kusikia mengi yanayomkera mtoto. Kuwa mwenye huruma na umwonyeshe kuwa unajali na kutafakari hali yake.

Ni vizuri kumsikiliza mtoto. Msikilize kwa makini na utulivu na hamu kuu. Kuwa na uwazi na mapenzi. Epuka kuwa na tamaa ya kuhukumu, kumkemea ama kusema vile unafikiri mtoto anafaa kufanya. Hapo wazo ni kuzipa hisia za mtoto nafasi ya kusikika. Jaribu kupata habari yote kwa njia ya usaili.

5. Kwa nini ni vibaya kutoa hukumu kwa mtoto?

  1. AHajafanya kosa lolote
  2. BMzazi si hakimu
  3. CUnaweza kumkasirisha zaidi
  4. DMtoto anaweza kuchelea kueleza hisia zake

Answer

D. Mtoto anaweza kuchelea kueleza hisia zake

Lengo ni "kuzipa hisia za mtoto nafasi ya kusikika"; hukumu humfanya aogope kusema.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test