CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1
Msukumo ambao unaweza kuwazidi watoto huletwa na nini hasa kulingana na ufahamu?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali la 1 - 7.
Mambo yanayohusu shule na maisha ya kijamii yanaweza wakati mwingine kuchangia msukumo ambao unaweza kuwazidi watoto. Lakini wanaweza kusaidiwa kujenga njia nzuri za kukabiliana na msongo na kusuluhisha shida zao kila siku.
Shirika moja la utafiti kule marekani linasema kuwa watoto husuluhisha msongo kwa njia nzuri au mbaya. Pia laelezea kuwa huku wakiwa hawawezi kuzungumzia kile kinachowasumbua watoto hutaka kuwafikia wazazi wao ili kupata msaada kushinda matatizo yao. Kwa kawaida si rahisi kwa wazazi kujua wafanye nini watoto wao wanaposhikwa na msongo.
Ni vyema kumwambia mtoto kuwa umegundua jambo ambalo linamsumbua. Ikiwezekana, taja hisia ambazo unadhani zinamtatiza mtoto. Hii haifai kuwa kama shutuma. Hii ni njia ya kawaida ya mtazamo kuwa unavutiwa na kutaka kusikia mengi yanayomkera mtoto. Kuwa mwenye huruma na umwonyeshe kuwa unajali na kutafakari hali yake.
Ni vizuri kumsikiliza mtoto. Msikilize kwa makini na utulivu na hamu kuu. Kuwa na uwazi na mapenzi. Epuka kuwa na tamaa ya kuhukumu, kumkemea ama kusema vile unafikiri mtoto anafaa kufanya. Hapo wazo ni kuzipa hisia za mtoto nafasi ya kusikika. Jaribu kupata habari yote kwa njia ya usaili.
1. Msukumo ambao unaweza kuwazidi watoto huletwa na nini hasa kulingana na ufahamu?
- AMambo yanayohusu dini na shule.
- BMambo yanayohusu umri na dini.
- CMambo yanayohusu maisha ya kijamii na shule.
- DMambo yasiyohusu shule na maisha ya kijamii.
Answer
C. Mambo yanayohusu maisha ya kijamii na shule.
"Mambo yanayohusu shule na maisha ya kijamii yanaweza … kuchangia msukumo."
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Shirika la utafiti lililotajwa katika taarifa ni la nchi gani?Question 2
- Watoto hutamani kuwafikia nani wanapozidiwa na hisia?Question 3
- Kushutumu ni kufanya nini?Question 4
- Kwa nini ni vibaya kutoa hukumu kwa mtoto?Question 5
- Mtoto anapomueleza mzazi shida zake mzazi anatakiwa kufanya haya yote isipokuwaQuestion 6
- Eleza maana ya usaili kama lilivyotumika katika taarifaQuestion 7