CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 3
ii. Eleza kwa nini Chepe alifanikiwa kumshinda zimwi Gogota. (Alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 2 marks · Topic: Fasihi, Hadithi
ZOEZI 2: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Hapo zamani za kale, katika kijiji cha Tambarare, aliishi shujaa aliyeitwa Chepe. Chepe alikuwa na nguvu za ajabu ambazo hazijawahi kuonekana; aliweza kung'oa mbuyu mkubwa kwa mikono yake miwili na kutembea nao kana kwamba ni unyasi. Kijiji kizima kilimtambua na kumtegemea kwa ulinzi.
Siku moja, zimwi la kutisha linalojulikana kama 'Gogota' lilivamia kijiji chao. Zimwi hilo lilikuwa na vichwa vitatu na lilitema moto mkali mdomoni. Lilianza kuharibu mimea, kuiba wanyama na kuwatia hofu wanakijiji. Hakuna shujaa yeyote aliyethubutu kulikabili, isipokuwa Chepe.
Chepe alichukua mkuki wake wa shaba na ngao yake ya ngozi ya kifaru, kisha akaelekea msituni kulikokuwa na pango la Gogota. Vita vilikuwa vikali, vumbi likatimka na kufunika jua. Kwa siku tatu mfululizo, walipigana bila mmoja kumshinda mwenzake. Hatimaye, Chepe alikumbuka siri aliyoambiwa na ajuza wa kijiji: udhaifu wa Gogota ulikuwa kwenye mkia wake mrefu.
Akitumia ujanja na wepesi kama wa chui, Chepe alikwepa mwali wa moto na kuukata mkia wa Gogota. Papo hapo, zimwi lile lilianguka chini kwa kishindo na kufariki. Chepe alirudi kijijini akiwa amembeba Gogota mabegani, na wanakijiji wakamlaki kwa nyimbo, vifijo na nderemo. Chepe akawa mkombozi wao na jina lake likaimbwa vizazi na vizazi.
ii. Eleza kwa nini Chepe alifanikiwa kumshinda zimwi Gogota. (Alama 2)
Answer
Alikumbuka siri aliyoambiwa na ajuza wa kijiji kwamba udhaifu wa Gogota uko kwenye mkia wake mrefu, akatumia ujanja na wepesi kuukata mkia huo.
Soma aya ya tatu na ya nne.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- iii. Eleza mandhari ya hadithi hii na jinsi inavyochangia kukuza hadithi yenyewe. (alama 2)Question 4
- iv. Eleza sifa mbili za Chepe kama zilivyojitokeza katika hadithi hii. (alama 2)Question 5
- v. Tambua na ueleze mbinu mbili za lugha zilizotumika katika kisa hiki. (Alama 2)Question 6
- i. Msuko ni mtiririko wa mawazo na maelezo katika kazi ya fasihi. Eleza msuko wa dondoo hili kwa aya moja tu. (alama 3)Question 7
- ii. Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika makala haya. (alama 4)Question 8
- iii. Taja na utoe mfano wa tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye kifungu hiki. (alama 2)Question 9