CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
i. Msuko ni mtiririko wa mawazo na maelezo katika kazi ya fasihi. Eleza msuko wa dondoo hili kwa aya moja tu. (alama 3)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 3 marks · Topic: Fasihi, Msuko
ZOEZI 3: FASIHI ANDISHI
NOVELA (ALAMA 10)
Soma dondo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
"Tazama jinsi mito ilivyokauka na wanyama wanavyoteseka," Mzee Tatu alisema huku akionyesha kwa kidole chake kilichokunjamana. "Haya yote ni matokeo ya tamaa yetu sisi binadamu. Tumekata miti yote tukitafuta utajiri wa haraka na sasa jua linatuchoma kama tanuri."
Kijana Sudi, ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini, aliinamisha kichwa kwa majuto. "Lakini babu, si tulihitaji mbao kujenga shule na nyumba zetu? Je, makosa yetu ni yepi haswa?"
"Makosa sio kujenga, mjukuu wangu. Kosa ni kutopanda mti mwingine pale unapokata mmoja. Maliasili ni kama akiba ya benki; ukitoa kila siku bila kuweka, ipo siku utabaki mikono mitupu. Sasa, mvua imetutoroka na njaa imetupiga kambi," Mzee Tatu alifafanua kwa sauti iliyojaa hekima na uchungu.
Sudi aliinua macho yake na kumtazama babu yake kwa uthabiti. "Nimeelewa. Kuanzia kesho, nitawakusanya vijana wenzangu. Tutaanza kampeni ya kupanda miche elfu moja kuzunguka kijiji chetu. Lazima tuokoe uhai wa ardhi yetu."
i. Msuko ni mtiririko wa mawazo na maelezo katika kazi ya fasihi. Eleza msuko wa dondoo hili kwa aya moja tu. (alama 3)
Answer
Mzee Tatu anamweleza mjukuu wake Kijana Sudi jinsi tamaa ya binadamu ya kukata miti bila kupanda mingine imesababisha ukame na njaa. Sudi anapata mwamko na kuamua kuwahamasisha vijana kuanzisha kampeni ya kupanda miche elfu moja ili kuokoa ardhi yao.
Anza na maelezo ya Mzee Tatu, malizia na uamuzi wa Sudi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- ii. Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika makala haya. (alama 4)Question 8
- iii. Taja na utoe mfano wa tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye kifungu hiki. (alama 2)Question 9
- iv. Ni sifa gani ya Mzee tatu iliyomfanya Kijana Sudi kumsikiliza kwa makini na baadaye kuchukua hatua ya kuokoa uhai…Question 10
- i. Maelekezo ya jukwaani ni mojawapo ya sifa za tamthilia. Eleza umuhimu wake ukirejelea dondoo hili. (alama 2)Question 11
- ii. Jadili maudhui makuu yanayojitokeza waziwazi katika dondoo hili. (alama 2)Question 12
- iii. Eleza sifa mbili za mhusika Bi. Rehema kama zilivyojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)Question 13