CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9
iii. Taja na utoe mfano wa tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye kifungu hiki. (alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 2 marks · Topic: Fasihi, Tamathali za Usemi
ZOEZI 3: FASIHI ANDISHI
NOVELA (ALAMA 10)
Soma dondo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
"Tazama jinsi mito ilivyokauka na wanyama wanavyoteseka," Mzee Tatu alisema huku akionyesha kwa kidole chake kilichokunjamana. "Haya yote ni matokeo ya tamaa yetu sisi binadamu. Tumekata miti yote tukitafuta utajiri wa haraka na sasa jua linatuchoma kama tanuri."
Kijana Sudi, ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini, aliinamisha kichwa kwa majuto. "Lakini babu, si tulihitaji mbao kujenga shule na nyumba zetu? Je, makosa yetu ni yepi haswa?"
"Makosa sio kujenga, mjukuu wangu. Kosa ni kutopanda mti mwingine pale unapokata mmoja. Maliasili ni kama akiba ya benki; ukitoa kila siku bila kuweka, ipo siku utabaki mikono mitupu. Sasa, mvua imetutoroka na njaa imetupiga kambi," Mzee Tatu alifafanua kwa sauti iliyojaa hekima na uchungu.
Sudi aliinua macho yake na kumtazama babu yake kwa uthabiti. "Nimeelewa. Kuanzia kesho, nitawakusanya vijana wenzangu. Tutaanza kampeni ya kupanda miche elfu moja kuzunguka kijiji chetu. Lazima tuokoe uhai wa ardhi yetu."
iii. Taja na utoe mfano wa tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye kifungu hiki. (alama 2)
Answer
Tashbihi: "jua linatuchoma kama tanuri". Sitiari: "njaa imetupiga kambi".
Tafuta ulinganisho kwa "kama" na bila "kama".
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- iv. Ni sifa gani ya Mzee tatu iliyomfanya Kijana Sudi kumsikiliza kwa makini na baadaye kuchukua hatua ya kuokoa uhai…Question 10
- i. Maelekezo ya jukwaani ni mojawapo ya sifa za tamthilia. Eleza umuhimu wake ukirejelea dondoo hili. (alama 2)Question 11
- ii. Jadili maudhui makuu yanayojitokeza waziwazi katika dondoo hili. (alama 2)Question 12
- iii. Eleza sifa mbili za mhusika Bi. Rehema kama zilivyojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)Question 13
- iv. Eleza dhamira ya mwandishi katika dondooo hili. (alama2)Question 14
- v. Taja na utolee mifano tamathali mbili za lugha zilizojitokeza katika dondoo hili. ( alama 2)Question 15