naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 14

iv. Eleza dhamira ya mwandishi katika dondooo hili. (alama2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 2 marks · Topic: Fasihi, Dhamira

ZOEZI 4: FASIHI ANDISHI
TAMTHILIA (ALAMA 10)
Soma sehemu ifuatayo kisha ujibu maswali.
(Ni sebuleni. Runinga inawaka lakini sauti iko chini. Kijana Jeni ameketi kitini, anabonyeza simu yake kwa kasi. Mama yake, Bi. Rehema, anaingia akiwa amebeba kikapu na kuonekana mchovu.)
Bi. Rehema: (Akiweka kikapu chini kwa hasira) Jeni! Tangu asubuhi uko kwenye hiyo simu. Hata vyombo hujapanga? Shule imefungwa lakini wewe kazi yako ni mtandao tu!
Jeni: (Bila kuinua uso) Mama, subiri kidogo. Nazungumza na rafiki yangu mpya niliyemjua mtandaoni. Ananiambia jinsi ya kupata pesa haraka kwa kutuma taarifa zangu za benki.
Bi. Rehema: (Anashtuka na kumsogelea Jeni haraka) Pesa haraka? Taarifa za benki? Wewe mtoto unataka kutuletea janga! Hujui kuwa kuna matapeli na uhalifu mwingi mtandaoni siku hizi?
Jeni: (Anainua uso sasa, akionyesha kuchanganyikiwa) Lakini alisema anafanya kazi kwenye shirika kubwa la kimataifa. Alinitumia hata picha yake!
Bi. Rehema: Picha si ushahidi! Vifaa vya kidijitali vina faida kubwa tukivitumia kwa mawasiliano mema na masomo, lakini ukiwapa watu usiowajua taarifa zako za siri, unawaalika wezi sebuleni kwetu.
Jeni: (Kwa aibu, anaweka simu chini) Samahani mama. Sikuwa na habari. Sitamtumia chochote. Nafikiri ni bora nimzuie kuwasiliana nami tena.

iv. Eleza dhamira ya mwandishi katika dondooo hili. (alama2)

Answer

Kuonya jamii, hasa vijana, kuhusu hatari za utapeli mtandaoni na kuhimiza matumizi salama ya vifaa vya kidijitali.

Mwandishi anataka tujifunze nini?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test