naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 5

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. MABADILIKO Mabadiliko lazima, kwa watu ulimwenguni, Nalo lilianza zama, hakika si neno geni, Ni tabia ya daima,…

From Kiswahili Karatasi ya 2 · 5 marks · Topic: Sehemu B — Shairi

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
MABADILIKO
Mabadiliko lazima, kwa watu ulimwenguni,
Nalo lilianza zama, hakika si neno geni,
Ni tabia ya daima, kipya kuwa cha zamani,
Kwa watu ulimwenguni, mabadiliko lazima.
Kama hili halikuwa, jipya lingekuja lini?
Mfano wetu maua, na majani ya mitini,
Hili linapofumuka, lile huanguka chini,
Jipya lingekuja lini, kama hili halikuwa?
Kuwapo na kutokuwapo, tumo mabadilikoni,
Nakuapia kiapo, kwamba hii ni kanuni,
Nawe linganisha pepo, kaskazi na kusini,
Tumo mabadilikoni, kuwapo na kutokuwapo.
Tukitaka tusitake, ni sheria tumo ndani,
Waume na wanawake, roho zote kwa Manani,
Kubadili mwendo wake, dunia si yamkini,
Ni sheria tumo ndani, tukitaka tusitake.
(S. Robert)
(a) Taja dhamira kuu ya shairi hili. (Alama 1)

(b) Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza katika shairi hili. (Alama 1)

(c) Neno “Manani” limetumiwa katika shairi hili. Maana ya Manani ni ipi? (Alama 1)

(d) Andika vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa tatu. (Alama 1)

(e) Taja mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika shairi hili. (Alama 1)

Answer

(a) Mabadiliko hayaepukiki katika maisha. (b) Tunapaswa kukubali kuwa kipya hubadilika na kuwa cha zamani. (c) Manani ni Mungu. (d) Vina vya kati katika mishororo 1–4: -po, -po, -po, -ni. Vina vya mwisho: -ni, -ni, -ni, -po. (e) Takriri, kwa mfano “mabadiliko lazima”.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test