CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 4
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali. ONYESHO 1 (Ni pale pale ofisini mwa Mzee Majoka, wakifuatana.) Majoka: (Anasimama na kusafisha koo)…
From Kiswahili Karatasi ya 2 · 10 marks · Topic: Sehemu B — Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
ONYESHO 1
(Ni pale pale ofisini mwa Mzee Majoka, wakifuatana.)
Majoka: (Anasimama na kusafisha koo) Karibuni wangwana; viongozi wa usoni wa Sagamoyo. Hamjambo?
Tunu: Hatujambo. (Awa mhemko) Twataka utuambie kwa nini...
Majoka: Salamu kwanza, binti mdogo. Msalimie ami yako.
Tunu: Ami? Tangu lini ukawa ami yangu?
Majoka: Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.
Tunu: Usinitoneshe kidonda tafadhali. Aliye na kovu usidhani kapona. Mambo ya baba siyo yaliyonileta hapa. Kesi yake tulimaliza zamani, ikanilikomaza kabla ya wakati wangu, alhamdulillahi!
Majoka: Acha pupa, binti mdogo. Usiyabebe maisha kwa mbeleko, dunia haiishi leo. Yaliyopita si ndwele, tuyape mgongo. Kosa halitibiwi kwa kosa na kama kuna tatizo, tutalitatua. (Awa Sudi) Umefanya vizuri sana kuja.
Sudi: Mimi Sudi?
Majoka: Wewe Sudi, nilijua utafika. Naona niseme nanyi kila mmoja peke yake.
Tunu: La hasha! Sema nasi sote. Wataka kutugawa?
Sudi: (Amekereka) Ajenda yangu ndiyo yake.
Maswali
(a) Tambua mandhari ya dondoo hili. (Alama 1)
(b) Eleza umuhimu wa maelekezo ya jukwaani yaliyoandikwa katika mabano katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)
(c) Mwandishi ametumia mbinu mbalimbali za lugha katika sehemu hii ya tamthilia. Eleza mbinu tatu za lugha zilizotumiwa. (Alama 3)
(d) Eleza mbinu nyingine za kimtindo zilizotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)
Answer
(a) Ofisini mwa Mzee Majoka. (b) Maelekezo ya jukwaani yanaonyesha vitendo vya wahusika na jinsi wanavyosema au kuonyesha hisia. (c) Methali: “Yaliyopita si ndwele, tuyape mgongo”; tashbihi: “tulikuwa kama ndugu”; takriri ya jina “Sudi” katika mazungumzo. (d) Dayalojia kati ya Majoka, Tunu na Sudi; maelekezo ya jukwaani kama “Anasimama na kusafisha koo”; maswali yanayoonyesha mvutano kama “Wataka kutugawa?”; urejeshi wa maisha yaliyopita katika mazungumzo kuhusu marehemu baba ya Tunu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. MABADILIKO Mabadiliko lazima, kwa watu ulimwenguni, Nalo lilianza zama,…Question 5
- Maagizo (i) Inapendekezwa uchukue muda wa dakika 40 katika zoezi hili. (ii) Andika insha yenye maneno kati ya 300–350…Question 1
- Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali. Kiongozi wa Waimbaji: Bidii ee, bidii ee, Bidii ee, bidii ee, Ufugaji ee,…Question 2
- Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali. Chale alikubaliana na Sudi kwamba shughuli zote katika mazingira…Question 3