CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 2
Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali. Kiongozi wa Waimbaji: Bidii ee, bidii ee, Bidii ee, bidii ee, Ufugaji ee, ufugaji ee, Shambani jifunge masombo. Mifugo…
From Kiswahili Karatasi ya 2 · 10 marks · Topic: Sehemu B — Fasihi Simulizi
Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali.
Kiongozi wa Waimbaji:
Bidii ee, bidii ee,
Bidii ee, bidii ee,
Ufugaji ee, ufugaji ee,
Shambani jifunge masombo.
Mifugo izaane kwa wingi,
Ugoigoi ni kwa wenye njaa.
Usingizi, tazama,
Tazama, tazama.
Wote ee!
Aiyee, mifugo ee!
Aiyee, konde letu!
Aiyee, tushughulikie.
(a) Wimbo huu ni wa aina gani? (Alama 1)
(b) Eleza sifa tatu za wimbo wa aina hii zinazojitokeza katika wimbo huu. (Alama 3)
(c) Eleza shughuli mbili ambazo jamii katika wimbo huu inafanya ili kujipatia mapato. (Alama 2)
(d) Tambua makundi mawili ya watu wanaoashiriwa na shughuli zinazotajwa katika wimbo huu. (Alama 2)
(e) Wimbo huu umewasilishwa na wenzenu darasani. Tambua mafunzo mawili yanayotokana na wimbo huu. (Alama 2)
Answer
(a) Wimbo wa kazi. (b) Una takriri, kwa mfano “bidii ee”; unahimiza bidii na kukataa ugoigoi; una mpokezano wa kiongozi na waimbaji wote. (c) Ufugaji wa mifugo na kilimo shambani. (d) Wafugaji na wakulima. (e) Tufanye kazi kwa bidii; tushirikiane kutunza mashamba na mifugo.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali. Chale alikubaliana na Sudi kwamba shughuli zote katika mazingira…Question 3
- Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali. ONYESHO 1 (Ni pale pale ofisini mwa Mzee Majoka, wakifuatana.)…Question 4
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. MABADILIKO Mabadiliko lazima, kwa watu ulimwenguni, Nalo lilianza zama,…Question 5
- Maagizo (i) Inapendekezwa uchukue muda wa dakika 40 katika zoezi hili. (ii) Andika insha yenye maneno kati ya 300–350…Question 1