naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 3

Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali. Chale alikubaliana na Sudi kwamba shughuli zote katika mazingira haya ziwe za kuhesabika. Baada ya kufanya…

From Kiswahili Karatasi ya 2 · 10 marks · Topic: Sehemu B — Novela

Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Chale alikubaliana na Sudi kwamba shughuli zote katika mazingira haya ziwe za kuhesabika. Baada ya kufanya aliyotakiwa kufanya, Sudi alimweleza Chale namna ya kukiwasha kile kiruninga kilichokuwa chumbani. Ni kweli kwamba pamoja na vipawa alivyokuwa navyo mtoto huyu, wakati mwingine baadhi ya runinga zilimtatiza.
Atajuaje kuziwasha ilhali kwao kulikuwa na redio tu? Mara moja moja alipofanikiwa kutumia runinga ilikuwa wakati alipokuwa kwa jirani yao. Sudi alimuaga Chale na kumwambia kwamba angerudi hivi punde kumpa dawa.
“Amenipa angalau muda wa kupumua kidogo. Naona karibu saa saba inakaribia. Acha nikiwashe nisikilize taarifa ya habari. Mguu huu umenifungia mengi. Siamini kwamba Jumapili ilinipita kama upepo. Sijui wenzangu walifanya nini kule Mpingoni. Shughuli ya kuogelea huenda haikufurahisha kama siku nyingine. Nasikitika kwamba hapajatokea yeyote mwingine mwenye hamu ya kujifunza utangazaji,” Chale alijisemea.
(a) Eleza aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)

(b) Eleza sifa mbili za Chale zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)

(c) Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)

(d) Eleza masuala mawili yanayojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)

Answer

(a) Mandhari ya mahali: chumbani, ambamo Sudi anamwelekeza Chale kuwasha runinga. Mandhari ya wakati: karibu saa saba, anapotaka kusikiliza taarifa ya habari. Pia Mpingoni ni mahali panapokumbukwa kwa shughuli ya kuogelea. (b) Chale ana vipawa, kama msimulizi anavyosema; anatafakari maisha yake na shughuli alizokosa. (c) Tashbihi: “Jumapili ilinipita kama upepo”; swali la balagha: “Atajuaje kuziwasha ilhali kwao kulikuwa na redio tu?” (d) Changamoto ya kiafya inamzuia Chale kushiriki shughuli; suala la vipawa na kujifunza utangazaji linajitokeza.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test