CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 6
Neno “tija” lililotumiwa katika kifungu lina maana ya:
From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi
Je, umewahi kuwazia kuhusu usafi wa sehemu za umma? Ama tuseme mazingira yetu kwa jumla? Ama usafi wa kibinafsi? Usafi ni neno ambalo limetawala vinywa vya watu wengi.
Mazingira yanajumuisha makazi yetu, nchi kavu, majini na hata hewani. Manufaa atakayopata mwanadamu kutokana na mazingira yetu yanategemea namna anavyodumisha usafi.
Wazia namna hali ingekuwa bila miti, mito, maziwa, milima, mabonde na hata hewa safi. Yakini hali ingekuwa tata. Kwa mfano, maziwa yakichafuliwa pamoja na mito hali itakuwaje? Mazingira safi yana tija kubwa kwa binadamu. Maji huhitajika viwandani, kunyunyizia mimea, kunywewa na mifugo pamoja na binadamu na vilevile hutumika katika shughuli mbalimbali za nyumbani kama vile za upishi. Maji yasiyokuwa safi huhatarisha maisha.
Mazingira yetu huwa na miti ambayo hurembesha nchi, hutumiwa kwa ujenzi, kutengeneza dawa, huwa makao ya baadhi ya wanyama na vilevile huvuta mvua na kusafisha hewa. Miti huzuia mmomonyoko wa udongo.
Tusitupe taka ovyo wala vitu vinavyoweza kuchafua mazingira. Tukiendelea kufanya hivyo tutakuwa chachandu anayejipalia makaa. Ni muhimu kuthamini usafi wa mazingira.

- AHasara
- BFaida
- CGharama
- DShida
Answer
B. Faida
Jibu sahihi ni: Faida.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza:Question 7
- Je, unafikiri ni jambo gani lililosababisha kutengana kwa Kuku na Mwewe?Question 8
- Chagua tabia za Mwewe kulingana na kifungu hiki.Question 9
- Aya ya pili imebainisha kwamba:Question 10
- Kwa mujibu wa kifungu hiki, Mwewe:Question 11
- Ni funzo gani kuhusu ushawishi wa majirani linalotokana na kifungu hiki?Question 12