CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 24
Chagua methali inayofaa kujaza nafasi iliyoachwa kwenye kifungu.
From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi
(Gakano na Jamila wanakutana saa nne asubuhi nje ya duka la kuuza nguo.)
Gakano: (Kwa tabasamu) Hujambo rafiki yangu?
Jamila: (Akitikisa kichwa) Sijambo ndugu. Habari za utokako?
Gakano: Kwema, mahitaji ndiyo mengi. Riziki yote anayojitafutia mtu huyeyukia kukidhi mahitaji.
Jamila: Kwa kweli unapaswa [22] ili uweze kufanikiwa maishani. Ama vipi, Gakano?
Gakano: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Kweli kabisa. Kumbuka kuwa wahenga walisema [24].
Jamila: Umegonga ndipo. Hakika usipojiwekea akiba utajipata pabaya. Juzi mtoto wa jirani alitumwa karo shilingi elfu tano. Akaona mwokozi ni mimi. Nilihuzunika sana. Baada ya kunieleza hali yake na uchochole wa wazazi wake, niliingia kwenye akiba yangu na kumpatia hela hizo. Alinishukuru na akatoka mbio kuelekea shuleni.
Gakano: Mungu akujalie. Kuna familia zinazojiweza kifedha.
Jamila: Naam!
Gakano: Wasemao babu umebarikiwa sana.
Jamila: (Kwa furaha) Hakika.

- AEnye miti hakuna wajenzi.
- BGuzo moja haijengi nyumba.
- CAkiba haiozi.
- DHaraka haraka haina baraka.
Answer
C. Akiba haiozi.
Jibu sahihi ni: Akiba haiozi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ni kipengele gani cha kusikiliza na kuzungumza ambacho hakijabainika katika mazungumzo haya?Question 25
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 27.Question 27
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 28.Question 28
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 29.Question 29
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 30.Question 30