naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 25

Ni kipengele gani cha kusikiliza na kuzungumza ambacho hakijabainika katika mazungumzo haya?

From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi

(Gakano na Jamila wanakutana saa nne asubuhi nje ya duka la kuuza nguo.)
Gakano: (Kwa tabasamu) Hujambo rafiki yangu?
Jamila: (Akitikisa kichwa) Sijambo ndugu. Habari za utokako?
Gakano: Kwema, mahitaji ndiyo mengi. Riziki yote anayojitafutia mtu huyeyukia kukidhi mahitaji.
Jamila: Kwa kweli unapaswa [22] ili uweze kufanikiwa maishani. Ama vipi, Gakano?
Gakano: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Kweli kabisa. Kumbuka kuwa wahenga walisema [24].
Jamila: Umegonga ndipo. Hakika usipojiwekea akiba utajipata pabaya. Juzi mtoto wa jirani alitumwa karo shilingi elfu tano. Akaona mwokozi ni mimi. Nilihuzunika sana. Baada ya kunieleza hali yake na uchochole wa wazazi wake, niliingia kwenye akiba yangu na kumpatia hela hizo. Alinishukuru na akatoka mbio kuelekea shuleni.
Gakano: Mungu akujalie. Kuna familia zinazojiweza kifedha.
Jamila: Naam!
Gakano: Wasemao babu umebarikiwa sana.
Jamila: (Kwa furaha) Hakika.

Ni kipengele gani cha kusikiliza na kuzungumza ambacho hakijabainika katika mazungumzo haya?

  1. AKuuliza na kujibu maswali
  2. BKuzungumza kwa zamu
  3. CMatumizi ya ishara za mwili
  4. DKuchachawizana wakati wa mazungumzo

Answer

D. Kuchachawizana wakati wa mazungumzo

Jibu sahihi ni: Kuchachawizana wakati wa mazungumzo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test