naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 23

Ni jambo gani ambalo Jamila anasisitiza kwa kusema “usipojiwekea akiba utajipata pabaya”?

From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi

(Gakano na Jamila wanakutana saa nne asubuhi nje ya duka la kuuza nguo.)
Gakano: (Kwa tabasamu) Hujambo rafiki yangu?
Jamila: (Akitikisa kichwa) Sijambo ndugu. Habari za utokako?
Gakano: Kwema, mahitaji ndiyo mengi. Riziki yote anayojitafutia mtu huyeyukia kukidhi mahitaji.
Jamila: Kwa kweli unapaswa [22] ili uweze kufanikiwa maishani. Ama vipi, Gakano?
Gakano: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Kweli kabisa. Kumbuka kuwa wahenga walisema [24].
Jamila: Umegonga ndipo. Hakika usipojiwekea akiba utajipata pabaya. Juzi mtoto wa jirani alitumwa karo shilingi elfu tano. Akaona mwokozi ni mimi. Nilihuzunika sana. Baada ya kunieleza hali yake na uchochole wa wazazi wake, niliingia kwenye akiba yangu na kumpatia hela hizo. Alinishukuru na akatoka mbio kuelekea shuleni.
Gakano: Mungu akujalie. Kuna familia zinazojiweza kifedha.
Jamila: Naam!
Gakano: Wasemao babu umebarikiwa sana.
Jamila: (Kwa furaha) Hakika.

Ni jambo gani ambalo Jamila anasisitiza kwa kusema “usipojiwekea akiba utajipata pabaya”?

  1. AKujiwekea akiba
  2. BMatumizi yafaayo ya pesa
  3. CKuwalipia watoto karo
  4. DNjia za kuondoa umaskini

Answer

A. Kujiwekea akiba

Jibu sahihi ni: Kujiwekea akiba.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test