naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 24

Amani alipotea akiwa na umri wa miaka mingapi?

From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 23 hadi 27.

(Asubuhi ya Jumamosi, Bi. Kendi alikuwa sokoni akinunua bidhaa za nyumbani. Ghafla, alisikia kilio cha mtoto mdogo. Aligeuka haraka kutafuta chanzo cha kilio hicho. Alimwona mtoto wa miaka minne akilia karibu na kibanda cha mboga.)

Bi. Kendi: (Akimkaribia mtoto) Pole sana, mwanangu. Mbona unalia?

Mtoto: (Akinuia machozi) Nimepotea, sijui mama yangu yuko wapi!

Bi. Kendi: Usijali, nitakusaidia. Unaitwa nani?

Mtoto: Ninaitwa Amani.

Bi. Kendi: Unamjua jina la mama yako?

Mtoto: Ndiyo, anaitwa Mama Amani.

Bi. Kendi: Sawa, hebu tuketi hapa kando ya duka hili. Huenda mama yako anatafuta mahali ulipopotea.

(Baada ya muda mfupi, mwanamke mmoja alifika akionekana mwenye wasiwasi.)

Mama Amani: (Kwa haraka) Mwanangu! Ulikuwa wapi? Nimekutafuta kila mahali!

Amani: (Akimkimbilia mamake) Mama! Nilikupoteza nikashindwa wapi pa kwenda.

Mama Amani: Asante sana, mama! Ulivyo mwema!

Bi. Kendi: Usijali, ni wajibu wetu kusaidiana. (Wanashikana mikono kwa furaha.)

24. Amani alipotea akiwa na umri wa miaka mingapi?

  1. AMiaka mitano.
  2. BMiaka mitatu.
  3. CMiaka minne.
  4. DMiaka sita.

Answer

C. Miaka minne.

Maelezo ya mwanzo yanasema alimwona mtoto wa miaka minne.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test