CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 30
Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 30.
From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ujazaji wa Nafasi (Kiswahili Sanifu)
Soma kifungu kifuatacho kisha jaza nafasi 28 hadi 37 kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwa majibu yaliyotolewa.
Katika jamii yoyote, mshikamano ni ....28.... kwa maendeleo. Watu wanapaswa ....29.... kwa amani na kushirikiana kwa hali na mali. Viongozi wa jamii ....30.... kuhakikisha kuwa wanachama wote wa jamii wanazingatia maadili mema. Ikiwa kuna ....31.... yoyote kati ya watu, wanapaswa kuzungumza na kutatua tofauti zao kwa njia ya ....32.....
Pia, ni muhimu kwa jamii kuzingatia usafi wa mazingira. ....33...., uchafu unaweza kusababisha magonjwa hatari kama vile kipindupindu. Watu wanapaswa kuwa na tabia ya kutupa taka ....34..... Aidha, wanajamii wanapaswa kupanda miti ....35.... hewa safi.
Wazazi wana jukumu muhimu katika ....36.... maadili mema kwa watoto wao. Watoto wakielimishwa vyema, basi jamii ....37.... mustakabali bora.
30. Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 30.
- AWanapaswa
- BWanapenda
- CWatatakiwa
- DWangepaswa
Answer
A. Wanapaswa
Viongozi wa jamii wanapaswa kuhakikisha kuwa maadili mema yanazingatiwa: ni wajibu wao.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 31.Question 31
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 32.Question 32
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 33.Question 33
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 34.Question 34
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 35.Question 35
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 36.Question 36