naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 28

Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 28.

From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ujazaji wa Nafasi (Kiswahili Sanifu)

Soma kifungu kifuatacho kisha jaza nafasi 28 hadi 37 kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwa majibu yaliyotolewa.

Katika jamii yoyote, mshikamano ni ....28.... kwa maendeleo. Watu wanapaswa ....29.... kwa amani na kushirikiana kwa hali na mali. Viongozi wa jamii ....30.... kuhakikisha kuwa wanachama wote wa jamii wanazingatia maadili mema. Ikiwa kuna ....31.... yoyote kati ya watu, wanapaswa kuzungumza na kutatua tofauti zao kwa njia ya ....32.....

Pia, ni muhimu kwa jamii kuzingatia usafi wa mazingira. ....33...., uchafu unaweza kusababisha magonjwa hatari kama vile kipindupindu. Watu wanapaswa kuwa na tabia ya kutupa taka ....34..... Aidha, wanajamii wanapaswa kupanda miti ....35.... hewa safi.

Wazazi wana jukumu muhimu katika ....36.... maadili mema kwa watoto wao. Watoto wakielimishwa vyema, basi jamii ....37.... mustakabali bora.

28. Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 28.

  1. AMuhimu
  2. BDuni
  3. CHatarishi
  4. DWastani

Answer

A. Muhimu

Mshikamano ni muhimu kwa maendeleo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test