CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 38
e) Ni akina nani waliochangia zaidi katika uchafuzi wa mazingira kijijini?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
29) NOVELLA.
Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Gari liliteremka taratibu. Mela alitupa macho nje ili ayatazame mazingira tofauti kabisa na yale aliyoyazoea utotoni. Awali, kwenye mteremko huo kulikuwa na kichaka kikubwa ambacho kiliwaogofya kina Mela. Ilibidi wazazi wao wawasindikize watoto wadogo wakienda shuleni asubuhi au waandamane na ndugu zao wakubwa.
Walipofika kwenye daraja, Mela alizidi kupigwa na bumbuwazi. Mto Salama ambao ulikuwa na maporomoko ya ajabu na maji mengi haukuwepo tena. Mahali pale kilikuwepo kijito kidogo chenye maji ya kahawia. Mela alimgeukia mwenzake aliyeketi naye sako kwa bako akamsaili yaliyojiri.
“Mwenye macho haambiwi tazama. Hivi ndivyo mambo yalivyo sasa.” Mela akajibiwa. Alielezwa jinsi wawekezaji wa kibinafsi walivyojenga viwanda na kuanzisha shughuli za kilimo-biashara kandokando ya mto Salama. Mto wenyewe ulilipiza kisasi kwa kuwanyima maji ya kutumia.
“Siku hizi ni muhali kupata hata kisamaki kidogo katika mto Salama,” mwenzake akahitimisha kwa masikitiko makuu.
Mela aliwazia ya kule mjini alikotoka. Alikumbuka mabiwi ya takataka, kelele za magari, moshi wa magari na viwanda na mitaro ya maji taka.
“Hivi binadamu amejitia hamnazo kabisa na kuendelea kuangamiza mazingira yake kotekote? Hivi karibuni, itakuja kubainika kwake methali isemayo, mwiba wa kujichoma hauambiwi pole.” Akajipata akijisemea kimoyomoyo.
e) Ni akina nani waliochangia zaidi katika uchafuzi wa mazingira kijijini?
Answer
Wawekezaji wa kibinafsi, waliojenga viwanda na kuanzisha shughuli za kilimo-biashara kandokando ya mto Salama.
Mela alielezwa kuwa wawekezaji wa kibinafsi walijenga viwanda na kuanzisha kilimo-biashara kando ya mto, na mto ukaharibika.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini jogoo hakuwa na marafiki wengi?Question 1
- Kondoo aliishi vizuri na wanyama wengine shambani. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu.Question 2
- Nini kilimwokoa kondoo?Question 3
- Umejifunza nini kutokana na kifungu hiki?Question 4
- Jukumu la kudumisha usafi wa maeneo mbalimbali ni la nani?Question 5
- Wananchi wanawezaje kuonyesha uwajibikaji wao?Question 6