naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 2

Kondoo aliishi vizuri na wanyama wengine shambani. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu.

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 4.

Katika shamba la mkulima mmoja, walikuwemo kondoo na jogoo. Kondoo alipendwa na wanyama wengine humo shambani kutokana na upole, ukarimu na kujali maslahi ya wengine. Jogoo kwa upande mwingine, hakuwa na marafiki wengi kutokana na utukutu na majisifu yake. Lililowakera wenzake zaidi ni jinsi jogoo alivyofurahia masaibu ya wengine badala ya kuwasikitikia.

Siku moja, jogoo alimsikia mzee mwenye shamba akimwambia mkewe, “Mke wangu, wazazi na ndugu zako wametuma taarifa kwamba watatutembelea juma lijalo. Unajua wale ni wakwe zangu. Sitaki wanichukulie kama mwenye mkono birika. Itabidi tumchinje kondoo ili wageni washibe kitoweo. Au waonaje?”

Mke aliafikiana na wazo hilo. Basi kutoka hapo, jogoo alienda himahima akawatangazia wanyama wote kuwa kondoo angewaacha juma ambalo lingefuata. Hakujali kuwa maneno yake yaliumiza hisia za kondoo na wote waliomjali.

Licha ya kujawa na huzuni moyoni, kondoo alimwomba Muumba wake huku akiamini kuwa mcha Mungu si mtovu. Jogoo naye alizoea kuamka mapema na kumkumbusha kondoo siku alizokuwa nazo za kuishi. Hata siku tatu kabla ya miadi, wageni walituma ujumbe kuwahakikishia wenyeji kuwa ugeni wao ungalipo. Nusura kondoo akate tamaa lakini akazidi kuomba.

Mkesha wa siku iliyotarajiwa, walikuja wageni wawili wakaeleza kuwa babamkwe wa mzee yule alikuwa ameugua ghafla na kulazwa hospitalini. Kwa hivyo, safari ilikuwa imevunjiliwa mbali. Alipanga kuandamana nao siku ambayo ingefuata ili akamjulie hali mgonjwa huyo. Licha ya kunusurika, kondoo alihuzunishwa sana na kifo cha jogoo.

2) Kondoo aliishi vizuri na wanyama wengine shambani. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu.

Answer

Kondoo alipendwa na wanyama wengine kutokana na upole, ukarimu na kujali maslahi ya wengine.

Aya ya kwanza inasema kondoo alipendwa na wanyama wengine kwa sababu ya upole, ukarimu na kujali maslahi ya wengine.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test