CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 33
b) Suala la uchafuzi wa mazingira limeangaziwa katika dondoo hili. Eleza mifano miwili ya jinsi binadamu anavyochafua mazingira kulingana na dondoo hili.
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
29) NOVELLA.
Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Gari liliteremka taratibu. Mela alitupa macho nje ili ayatazame mazingira tofauti kabisa na yale aliyoyazoea utotoni. Awali, kwenye mteremko huo kulikuwa na kichaka kikubwa ambacho kiliwaogofya kina Mela. Ilibidi wazazi wao wawasindikize watoto wadogo wakienda shuleni asubuhi au waandamane na ndugu zao wakubwa.
Walipofika kwenye daraja, Mela alizidi kupigwa na bumbuwazi. Mto Salama ambao ulikuwa na maporomoko ya ajabu na maji mengi haukuwepo tena. Mahali pale kilikuwepo kijito kidogo chenye maji ya kahawia. Mela alimgeukia mwenzake aliyeketi naye sako kwa bako akamsaili yaliyojiri.
“Mwenye macho haambiwi tazama. Hivi ndivyo mambo yalivyo sasa.” Mela akajibiwa. Alielezwa jinsi wawekezaji wa kibinafsi walivyojenga viwanda na kuanzisha shughuli za kilimo-biashara kandokando ya mto Salama. Mto wenyewe ulilipiza kisasi kwa kuwanyima maji ya kutumia.
“Siku hizi ni muhali kupata hata kisamaki kidogo katika mto Salama,” mwenzake akahitimisha kwa masikitiko makuu.
Mela aliwazia ya kule mjini alikotoka. Alikumbuka mabiwi ya takataka, kelele za magari, moshi wa magari na viwanda na mitaro ya maji taka.
“Hivi binadamu amejitia hamnazo kabisa na kuendelea kuangamiza mazingira yake kotekote? Hivi karibuni, itakuja kubainika kwake methali isemayo, mwiba wa kujichoma hauambiwi pole.” Akajipata akijisemea kimoyomoyo.
b) Suala la uchafuzi wa mazingira limeangaziwa katika dondoo hili. Eleza mifano miwili ya jinsi binadamu anavyochafua mazingira kulingana na dondoo hili.
Answer
Kujenga viwanda kando ya mto Salama kumefanya maji yake kuwa ya kahawia. Mjini kuna mabiwi ya takataka na moshi wa magari na viwanda.
Dondoo linaonyesha uchafuzi kijijini (viwanda na kilimo-biashara kando ya mto, maji ya kahawia) na mjini (takataka, kelele, moshi na mitaro ya maji taka).
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- c) Mwandishi wa dondoo hili ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Kauli ifuatayo imetumia tamathali gani ya usemi? i.…Question 34
- Kauli ifuatayo imetumia tamathali gani ya usemi? ii. Mwenye macho haambiwi tazamaQuestion 35
- Kauli ifuatayo imetumia tamathali gani ya usemi? iii. Mto wenyewe ulilipiza kisasi kwa kuwanyima maji ya kutumiaQuestion 36
- d) Eleza hali ilivyokuwa Mela alipokuwa mtoto.Question 37
- e) Ni akina nani waliochangia zaidi katika uchafuzi wa mazingira kijijini?Question 38
- Kwa nini jogoo hakuwa na marafiki wengi?Question 1