naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 32

a) Andika aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika dondoo hili.

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela

29) NOVELLA.
Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Gari liliteremka taratibu. Mela alitupa macho nje ili ayatazame mazingira tofauti kabisa na yale aliyoyazoea utotoni. Awali, kwenye mteremko huo kulikuwa na kichaka kikubwa ambacho kiliwaogofya kina Mela. Ilibidi wazazi wao wawasindikize watoto wadogo wakienda shuleni asubuhi au waandamane na ndugu zao wakubwa.

Walipofika kwenye daraja, Mela alizidi kupigwa na bumbuwazi. Mto Salama ambao ulikuwa na maporomoko ya ajabu na maji mengi haukuwepo tena. Mahali pale kilikuwepo kijito kidogo chenye maji ya kahawia. Mela alimgeukia mwenzake aliyeketi naye sako kwa bako akamsaili yaliyojiri.

“Mwenye macho haambiwi tazama. Hivi ndivyo mambo yalivyo sasa.” Mela akajibiwa. Alielezwa jinsi wawekezaji wa kibinafsi walivyojenga viwanda na kuanzisha shughuli za kilimo-biashara kandokando ya mto Salama. Mto wenyewe ulilipiza kisasi kwa kuwanyima maji ya kutumia.

“Siku hizi ni muhali kupata hata kisamaki kidogo katika mto Salama,” mwenzake akahitimisha kwa masikitiko makuu.

Mela aliwazia ya kule mjini alikotoka. Alikumbuka mabiwi ya takataka, kelele za magari, moshi wa magari na viwanda na mitaro ya maji taka.

“Hivi binadamu amejitia hamnazo kabisa na kuendelea kuangamiza mazingira yake kotekote? Hivi karibuni, itakuja kubainika kwake methali isemayo, mwiba wa kujichoma hauambiwi pole.” Akajipata akijisemea kimoyomoyo.

a) Andika aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika dondoo hili.

Answer

Mandhari ya kijijini (mto Salama na daraja) na mandhari ya mjini alikotoka Mela.

Matukio yanatokea kijijini Mela anaporudi (mteremko, daraja, mto Salama), na Mela anakumbuka mjini alikotoka (mabiwi ya takataka, kelele na moshi).

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test