naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 10

Tabia gani ya kobe ilisababisha aonekane mbaya baadaye?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma ufahamu huu kisha ujibu swali 8 hadi 13.
Zamani za kale, wanyama wote walikuwa na ngozi laini kama ya mtoto mchanga. Kobe alikuwa miongoni mwa waliokuwa warembo zaidi. Alipenda kujigamba kuhusu mwonekano wake mbele ya wenzake hasa ndege waliokuwa na manyoya ya kuvutia.
Siku moja, kunguru alialikwa kwenye sherehe mbinguni. Kobe naye akataka kwenda naye lakini hakuwa na mbawa. Alimwomba kunguru amsaidie. Kunguru kwa hila alimpa baadhi ya manyoya ya wanyama wengine. Kobe alijibamba na kupaa mbinguni akiwa na furaha.
Katika sherehe, alikula chakula kingi kuliko wote na hata kuanza kuwakejeli waliomsaidia. Wenyeji walikasirika, wakamwondoa kwa nguvu. Alipotupwa kutoka mbinguni alianguka na kuvunjika vibaya.
Aliokolewa lakini sura yake haikurudi kama hapo awali. Ndipo akaanza kuvaa gomba kumkinga. Tangu siku hiyo, kobe amekuwa na mogamba yanayofunika mwili wake kama kumbikumbi ya kiburi na dharau zake.

10. Tabia gani ya kobe ilisababisha aonekane mbaya baadaye?

  1. AHasira ya chuki
  2. BKutokuoga
  3. CKiburi na dharau
  4. DKupenda kula sana

Answer

C. Kiburi na dharau

Gamba ni kumbukumbu ya kiburi na dharau zake.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test