CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9
Wengine hawakukaa sebuleni kwa sababu
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali la 8 hadi 13.
Wageni tuliowaalika kutoka Ugiriki walituwekea masharti magumu. Walikataa katakata kuchukuliwa hotelini au kuletewa chakula cha hoteli. Tukakubali kwa kuwa hatukuwa na budi.
Walipofika tu, walijigawa, wengine wakabaki sebuleni na wengine wakaenda moja kwa moja hadi jikoni. Do! Kumbe kilichowaleta mapema mno ni kutaka kuona mapishi yetu.
Kwa hakika walituwahi vizuri. Mimi binafsi nilikuwa na kinu na mchi nikitwanga maharagwe. Shangazi alikuwa juu ya mbuzi akikuna nazi huku malkia akimsaidia kuichuja nazi hiyo kwa kifumbu ili apate tui na machicha. Halati akawa yuampara samaki huku Amati akiunga mchuzi kwa viungo alivyokuwa amevitayarisha. Nyanya alikuwa akidondoa mchele kuondoa ndume ilhali wifi zangu walikuwa wakiambua viazi, kuoka mikate na kukoka moto. Jirani yetu Bidii alikuwa akikanda unga na baadaye kuisukuma mikate.
9. Wengine hawakukaa sebuleni kwa sababu
- Anafasi haikutosha
- Bwaliamrishwa kwenda jikoni
- Cmila zao hazikuwaruhusu kukaa sebuleni
- Dwalitaka kujionea mapishi ya kiasili
Answer
D. walitaka kujionea mapishi ya kiasili
"Kilichowaleta mapema mno ni kutaka kuona mapishi yetu."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni nani aliyetumia bizari na tangawizi?Question 10
- Kifungu kukoka moto kimetumiwa katika ufahamu maana yake niQuestion 11
- Sentensi ipi si kweli?Question 12
- Ni nini maana ya “tukakubali kwa kuwa hatukuwa na budi?Question 13
- Kipwerere alikuwa na nywele za singa. Je, hizi ni nywele za aina gani?Question 14
- Kipwerere aliugua kwa muda waQuestion 15