CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 3
Ni kidole kipi hutumika sana kuwanyoshea watu?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma ufahamu ufuatao kisha jibu maswali 1 hadi 7.
Kidole kimoja hakivunji chawa. Ndivyo wasemavyo wahenga. Mkono wa mwanadamu una vidole vitano. Kidole kidogo, cha pete, cha kati, cha shahada na kidole gumba. Kati ya vidole hivi vyote, kidole cha shahada ndicho kinachotumiwa sana kwa mambo mengi. Kidole hiki hutumika kumwonya mtu. Si heshima wala adabu njema kwa mdogo kumnyoshea mkubwa wake kwa umri wa cheo kidole ili kumwonya. Kumbuka unapomnyoshea mtu kidole hicho cha shahada ili kumwonya vidole nyingine vitatu huwa vimekuelekea wewe mwenyewe kukuonya pia.
Baadhi ya watu hupenda kuwaita watu wengine kwa kidole cha shahada huku wakichezesha na kukielekeza kwao. Hiyo si tabia nzuri hata kidogo.
3. Ni kidole kipi hutumika sana kuwanyoshea watu?
- ACha pete
- BCha shahada
- CGumba
- DKidogo
Answer
B. Cha shahada
Kidole cha shahada hutumika kumwonya mtu.