naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Aisha na Juma waliamua kuanzisha nini?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Dayolojia

Soma dayologia ifuatayo kisha ujibu maswali. (Afya ni mali)
Asha: Habari ya asubuhi Juma?
Juma: Nzuri sana Asha, wewe je?
Asha: Nzuri pia, Nilikuona jana ukikimbia asubuhi. Unajitayarisha kwa michezo!
Juma: Ndio. Lakini pia nakimbia ili kudumisha afya yangu. Mwalimu wa Sayansi alisema mazoezi husaidia mwili kuwa imara.
Asha: Ni kweli kabisa, mimi hujaribu kula matunda kila siku. Mama alisema lishe bora ni muhimu kwa afya njema.
Juma: Hilo ni jambo nzuri. Watu wengi siku hizi hula vyakula vya mafuta kupita kiasi, kisha wanapata magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu.
Asha: Pia ni muhimu kunywa maji mengi na kupumzika vya kutosha. Wengi hukosa kulala vya kutosha kwa sababu ya simu na televisheni.
Juma: Nakubaliana nawe afya bora ni matokeo ya mazoezi, lishe bora na utunzaji wa mwili.
Asha: Hebu tuanzishe klabu ya afya shuleni ili kuelimisha wanafunzi wengine.
Juma: Wazo zuri! Tutaita afya yetu mali yetu.

5. Aisha na Juma waliamua kuanzisha nini?

  1. AKlabu ya michezo
  2. BKlabu ya afya
  3. CKlabu ya usafi
  4. DKlabu ya mali

Answer

B. Klabu ya afya

"Hebu tuanzishe klabu ya afya shuleni."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test