CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2
Asha hufanya nini ili kutunza afya yake?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Dayolojia
Soma dayologia ifuatayo kisha ujibu maswali. (Afya ni mali)
Asha: Habari ya asubuhi Juma?
Juma: Nzuri sana Asha, wewe je?
Asha: Nzuri pia, Nilikuona jana ukikimbia asubuhi. Unajitayarisha kwa michezo!
Juma: Ndio. Lakini pia nakimbia ili kudumisha afya yangu. Mwalimu wa Sayansi alisema mazoezi husaidia mwili kuwa imara.
Asha: Ni kweli kabisa, mimi hujaribu kula matunda kila siku. Mama alisema lishe bora ni muhimu kwa afya njema.
Juma: Hilo ni jambo nzuri. Watu wengi siku hizi hula vyakula vya mafuta kupita kiasi, kisha wanapata magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu.
Asha: Pia ni muhimu kunywa maji mengi na kupumzika vya kutosha. Wengi hukosa kulala vya kutosha kwa sababu ya simu na televisheni.
Juma: Nakubaliana nawe afya bora ni matokeo ya mazoezi, lishe bora na utunzaji wa mwili.
Asha: Hebu tuanzishe klabu ya afya shuleni ili kuelimisha wanafunzi wengine.
Juma: Wazo zuri! Tutaita afya yetu mali yetu.
2. Asha hufanya nini ili kutunza afya yake?
- AHula matunda kila siku
- BKufanya mazoezi asubuhi
- CHula siku nzima
- DHula sukari
Answer
A. Hula matunda kila siku
"Mimi hujaribu kula matunda kila siku."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni hatari gani zinazotokana na kula vyakula vya mafuta kupita kiasi?Question 3
- Kwanini watu wengi hukosa kulala vya kutosha?Question 4
- Aisha na Juma waliamua kuanzisha nini?Question 5
- Funzo la dayolojia hii ni lipi?Question 6
- Kijiji kinachozungumziwa katika hadithi kinaitwaje?Question 7
- Wanafunzi walipaswa kutumia tecknolojia kufanya nini?Question 8