CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 24
Ni nini maana ya nahau nitajifunga nira?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.
(Bi. Zawadi anamtembelea Juma, mwanafunzi wake baada ya kutohudhuria shule kwa muda mrefu.)
Bi. Zawadi : __21__! Sijakuona shuleni siku hizi. Kuna nini?
Juma : Karibu mwalimu. Pole sana kwa kukusumbua. Nimekuwa mgonjwa kwa muda, ndiyo maana sijaweza kuja shuleni.
Bi. Zawadi : Pole sana mwanangu. Nilitaka kujua hali yako. Wanafunzi wenzako wamekukosa sana darasani.
Juma : Nashukuru sana mwalimu. Nimelia sana kwa kukosa masomo. Ninahofia nitabaki nyuma.
Bi. Zawadi : Usijali Juma. Tutaangalia jinsi ya kukupatia masomo uliyokosa. Cha muhimu ni afya yako kwanza.
Juma : Asante mwalimu. Umekuwa msaada mkubwa kwangu. Ninakupenda sana.
Bi. Zawadi : Ni wajibu wangu kuhakikisha mnafanya vizuri. Kazi yangu ni kuwasaidia. Japo umekuwa mgonjwa, jinsi ulivyoweza leo, inaonyesha unaweza kufanya mambo makubwa.
Juma : Nitaendelea kujitahidi, mwalimu. Nitajifunga nira nikirudi kwani bidii hufaidi.
Bi. Zawadi : Vizuri sana Juma. Kumbuka achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
24. Ni nini maana ya nahau nitajifunga nira?
- ANitafanya kazi
- BNitakuwa mzembe
- CNitasoma sana
- DNitafanya bidii
Answer
D. Nitafanya bidii
Kujifunga nira ni kufanya bidii.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Achanikaye kwenye mpini hafi njaa ni methali inayohimizaQuestion 25
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 27.Question 27
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 28.Question 28
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 29.Question 29
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 30.Question 30