naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 23

Bi. Zawadi anasisitiza ni nini muhimu?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.
(Bi. Zawadi anamtembelea Juma, mwanafunzi wake baada ya kutohudhuria shule kwa muda mrefu.)
Bi. Zawadi : __21__! Sijakuona shuleni siku hizi. Kuna nini?
Juma : Karibu mwalimu. Pole sana kwa kukusumbua. Nimekuwa mgonjwa kwa muda, ndiyo maana sijaweza kuja shuleni.
Bi. Zawadi : Pole sana mwanangu. Nilitaka kujua hali yako. Wanafunzi wenzako wamekukosa sana darasani.
Juma : Nashukuru sana mwalimu. Nimelia sana kwa kukosa masomo. Ninahofia nitabaki nyuma.
Bi. Zawadi : Usijali Juma. Tutaangalia jinsi ya kukupatia masomo uliyokosa. Cha muhimu ni afya yako kwanza.
Juma : Asante mwalimu. Umekuwa msaada mkubwa kwangu. Ninakupenda sana.
Bi. Zawadi : Ni wajibu wangu kuhakikisha mnafanya vizuri. Kazi yangu ni kuwasaidia. Japo umekuwa mgonjwa, jinsi ulivyoweza leo, inaonyesha unaweza kufanya mambo makubwa.
Juma : Nitaendelea kujitahidi, mwalimu. Nitajifunga nira nikirudi kwani bidii hufaidi.
Bi. Zawadi : Vizuri sana Juma. Kumbuka achanikaye kwenye mpini hafi njaa.

23. Bi. Zawadi anasisitiza ni nini muhimu?

  1. AAfya yetu
  2. BElimu yetu
  3. CMafunzo yetu
  4. DMuda wetu

Answer

A. Afya yetu

"Cha muhimu ni afya yako kwanza."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test