CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8
b) Taja na uthibitishe mbinu mbili za uandishi ambazo zimetumika katika dondoo hili. (Alama 4)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 4 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Andishi
FASIHI ANDISHI (ALAMA 10)
Soma dondoo hili kutoka Mshale wa Matumaini kisha ujibu maswali.
.............Siku zilizidi kusonga tukiwa tunaishi kwa msaada wa chakula cha mgao kambini. Tuliishi kwa mchele na maharagwe au pojo na ngano.
Nilipenda kufukuza mawazo yangu kwa kucheza kandanda. Ningeenda uwanjani kucheza kandanda au kutazamia wenzangu wakicheza. Ingawa nilikuwa mchezaji mwenye uzoefu tokea nilipokuwa Doneka, hawakutaka nijumuike nao kuchezea timu yao. Baadhi waliniita muaji pale uwanjani. Nilishangaa kwa nini vijana wengine walikuwa wakinichukia bila sababu. Hata Deno alipunguza uhusiano wake na mimi. Nilichukia hali hiyo. Iliathiri masomo yangu kwa kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya walimu walishangaa kusikia kwamba nilikuwa mtoto wa jambazi sugu huko Doneka. Nilisikia kauli kama ‘mtoto we nyoka ni nyoka.’
Maisha ya Gera yalinikera sana. Nlitamani kurudi kwetu licha ya tabu zilizokuwepo. Nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni. Niliomba Mungu azidi kuonyesha wengine, Mzee Musambale akiwemo, tofauti kati yangu na Kadurenge, baba yangu. Maswali mengi kumhusu yalizuka. Kwa nini aliingia katika harakati kama hizo? Alikuwa amekosewa na nani? Ni nani aliyemuudhi? Mbona hakulalamikia vyombo vya usalama? Maswali haya na mengine yalinijia akilini. Nilipigana nayo kuyaelewa. Nilitamani mama yangu angekuwa hai anisaidie kuyajibu. Hata kama asingenisaidia angekuwa rafiki yangu wa karibu lakini hakuwepo sasa. Maisha yalisonga japo kwa dhiki nyingi.
b) Taja na uthibitishe mbinu mbili za uandishi ambazo zimetumika katika dondoo hili. (Alama 4)
Answer
Methali: "mtoto wa nyoka ni nyoka"; maswali ya balagha: "Kwa nini aliingia katika harakati kama hizo?"
Tafuta methali na maswali yasiyohitaji jibu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- c) Taja dhiki tatu alizopitia mwandishi wa dondoo hili kulingana na makala haya. (Alama 3)Question 9
- a) Malenga wa shairi hili ni nani? (Alama 1)Question 10
- b) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha (Alama 2)Question 11
- c) Andika kibwagizo cha shairi hili. (Alama 1)Question 12
- d) Je, mloto wa ubeti wa pili una mizani ngapi? (Alama 2)Question 13
- e) Andika vina vya ubeti wa kwanza. (Alama 2)Question 14