CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 1
Kulingana na aya ya kwanza, ni kauli gani inayoonyesha mipaka ya majukumu ya watoto katika jamii?
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
Kwa kweli, si jambo la mjadala kuwa jamii ina jukumu la kumlea mtoto. Hata hivyo, mtoto naye ana majukumu anuwai anayopaswa kuyatekeleza katika jamii yake. Mtoto anaposaidiwa, haifai ajipakatie mikono. Afanye juhudi kutekeleza majukumu yake ili anayemsaidia awe na sababu ya kuendelea kumsaidia. Vile vile, majukumu kwa mtoto yanapaswa kuzingatia hali na umri wake.
Watoto wanapaswa kujiunga na shule kwa wakati ufaao na kuendelea na masomo hadi watakapohitimu kiwango kinachostahili. Shuleni, watoto hawana budi kutii na kuzingatia masomo. Hili litamsaidia kupata stadi, ujuzi, maarifa, maadili na mielekeo inayofaa maishani.
Mtoto anapaswa kuwasaidia wazazi wake na kufanya kazi ndogo ndogo kulingana na umri wake. Anapofanya kazi hizo anapaswa kuwajibikia vifaa anavyotumia. Hii itamsaidia kuwa na uwajibikaji katika maisha yake.
Mbali na hayo, mtoto anapaswa kushirikiana na wenzake shuleni na hata katika jamii. Ashirikiane na wenzake katika ujifunzaji. Anapofanya hivyo, awe makini kuwateua marafiki wazuri. Mmoja akifanya jambo lisilofaa, amshauri abadilike; akishindwa, amwombe mwalimu msaada. Kwa kufanya hivyo, atakuwa amemsaidia mwenzake.
Watoto wanapaswa kujiunga na shule kwa wakati ufaao na kuendelea na masomo hadi watakapohitimu kiwango kinachostahili. Shuleni, watoto hawana budi kutii na kuzingatia masomo. Hili litamsaidia kupata stadi, ujuzi, maarifa, maadili na mielekeo inayofaa maishani.
Mtoto anapaswa kuwasaidia wazazi wake na kufanya kazi ndogo ndogo kulingana na umri wake. Anapofanya kazi hizo anapaswa kuwajibikia vifaa anavyotumia. Hii itamsaidia kuwa na uwajibikaji katika maisha yake.
Mbali na hayo, mtoto anapaswa kushirikiana na wenzake shuleni na hata katika jamii. Ashirikiane na wenzake katika ujifunzaji. Anapofanya hivyo, awe makini kuwateua marafiki wazuri. Mmoja akifanya jambo lisilofaa, amshauri abadilike; akishindwa, amwombe mwalimu msaada. Kwa kufanya hivyo, atakuwa amemsaidia mwenzake.
Kulingana na aya ya kwanza, ni kauli gani inayoonyesha mipaka ya majukumu ya watoto katika jamii?
- AKwa kuwachagua marafiki wazuri pekee.
- BWatoto wanapaswa kufanya kazi katika jamii bila masharti.
- CMtoto asilegee kazini kiasi cha kutaka kusaidiwa.
- DSi majukumu yote katika jamii yanayoweza kutekelezwa na watoto.
Answer
D. Si majukumu yote katika jamii yanayoweza kutekelezwa na watoto.
Aya ya kwanza inaeleza kuwa majukumu yanapaswa kuzingatia hali na umri wa mtoto; kwa hiyo si kila jukumu linafaa kwa watoto.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua methali inayoafikiana na maelezo ya aya ya kwanza.Question 2
- Majukumu ya watoto yanapaswa kuzingatia mambo gani?Question 3
- Kwa mujibu wa aya ya tatu, watoto wanapaswa kuchangia malezi kwa:Question 4
- Kwa kurejelea aya ya nne, chagua jibu linaloonyesha kuwa mtoto anapaswa kuwa na msimamo thabiti maishani.Question 5
- Chagua kisawe cha neno “kumshauri” kama lilivyotumiwa katika kifungu.Question 6
- Ni jambo gani linaloonyesha kuwa nchi ya Jijenge ilikuwa na utajiri mkubwa?Question 7