CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 6
Chagua kisawe cha neno “kumshauri” kama lilivyotumiwa katika kifungu.
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
Kwa kweli, si jambo la mjadala kuwa jamii ina jukumu la kumlea mtoto. Hata hivyo, mtoto naye ana majukumu anuwai anayopaswa kuyatekeleza katika jamii yake. Mtoto anaposaidiwa, haifai ajipakatie mikono. Afanye juhudi kutekeleza majukumu yake ili anayemsaidia awe na sababu ya kuendelea kumsaidia. Vile vile, majukumu kwa mtoto yanapaswa kuzingatia hali na umri wake.
Watoto wanapaswa kujiunga na shule kwa wakati ufaao na kuendelea na masomo hadi watakapohitimu kiwango kinachostahili. Shuleni, watoto hawana budi kutii na kuzingatia masomo. Hili litamsaidia kupata stadi, ujuzi, maarifa, maadili na mielekeo inayofaa maishani.
Mtoto anapaswa kuwasaidia wazazi wake na kufanya kazi ndogo ndogo kulingana na umri wake. Anapofanya kazi hizo anapaswa kuwajibikia vifaa anavyotumia. Hii itamsaidia kuwa na uwajibikaji katika maisha yake.
Mbali na hayo, mtoto anapaswa kushirikiana na wenzake shuleni na hata katika jamii. Ashirikiane na wenzake katika ujifunzaji. Anapofanya hivyo, awe makini kuwateua marafiki wazuri. Mmoja akifanya jambo lisilofaa, amshauri abadilike; akishindwa, amwombe mwalimu msaada. Kwa kufanya hivyo, atakuwa amemsaidia mwenzake.

- AKumsaidia
- BKumwelekeza
- CKumtunza
- DKumlinda
Answer
B. Kumwelekeza
Kumshauri ni kumwelekeza mtu kuhusu jambo analoweza kufanya.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni jambo gani linaloonyesha kuwa nchi ya Jijenge ilikuwa na utajiri mkubwa?Question 7
- Kifungu kimebainisha kuwa wanyama walijali maslahi ya wenzao. Chagua jibu linalothibitisha kauli hii.Question 8
- Kauli “yalipowafika kooni” imetumia mbinu gani ya lugha?Question 9
- Kama Kiboko hangefika ziwani, unadhani kungetokea nini?Question 10
- Kwa mujibu wa kifungu, Simba:Question 11
- Matukio yafuatayo yalitokea katika kifungu: i. Wanyama kutumia ziwa. ii. Kobe kumkanya Fisi. iii. Simba kuridhia…Question 12